Pages

Friday, May 1, 2015

THAMANI YA SHILINGI: Mtei aifunda Benki Kuu

Gavana wa kwanza wa Benki Kuu Tanzania, Edwin Mtei 
Na Mussa Juma, Mwananchi
Kwa ufupi
  • Abainisha namna ya kuinusuru shilingi, asema ni suala la kitaalamu zaidi, akemea siasa kuingilia suala hili.Share


Arusha. Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Edwin Mtei  ametoa somo kwa benki hiyo kuinusuru shilingi isiendelee kuporomoka kwa kutumia akiba ya fedha za kigeni ilizonazo.
Katika siku za karibuni, thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni, hasa dola, imeporomoka hadi kufikia Sh2010 kwa dola moja ya Marekani.
Akizungumza jana, Mtei alisema hakuna chombo kingine kinachoweza kusaidia tatizo hili zaidi ya Benki Kuu, kwa sasa.
“Hili ni suala la kitaalamu siyo la kisiasa, Benki Kuu lazima itumie wataalamu wake sasa, kuhakikisha wanailinda shilingi na hatuwezi kulalamikia mataifa ya nje katika hili,” alisema.
 Mtei ambaye alijiuzulu kutokana na mgogoro kama huu alisema, BoT ni lazima isaidie Serikali kudhibiti manunuzi nje ya nchi na itoe sehemu ya akiba yake ya fedha za kigeni.
“Mimi nilijiuzulu katika masuala haya ya thamani ya fedha yetu, tulitofautiana na Mwalimu Julius Nyerere,” alisema.
 Alisema anakumbuka wakati wa uongozi wao, waliwahi kushusha dola hadi kufikia Sh12 na hakuna chombo cha nje kilichowahi kulalamika kwani hili ni suala la ndani ya nchi.
Mshauri Mwandamizi wa Masuala ya Uchumi na Mipango mkoani Arusha, Saimon Mapolu akizungumzia kushuka kwa thamani ya shilingi alisema, inatokana na upungufu katika sera ya fedha na sheria zilizopo.
Mapolu, hata hivyo, alisema kwa hali ya sasa, BoT inaweza kudhibiti hali isiwe mbaya zaidi.
Alisema hakuna maana kuwa na akiba nyingi ya fedha za kigeni wakati shilingi ikiwa sio imara

No comments:

Post a Comment