Pages

Friday, February 22, 2013

NSSF yafafanua mikopo ya Saccos


Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde 

Posted  Alhamisi,Februari21  2013  saa 23:34 PM
Kwa ufupi

Akizungumza wakati wa kuutambulisha utaratibu huo kwa wafanyakazi wa Kamapuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Makao Makuu Tabata, Dar es Salaam jana, Meneja


UTARATIBU wa mikopo kwa Vyama vya Kuweka na Kukopa (Saccos) ambao unatekelezwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), umewalenga wanachama wa mfuko huo ili kuweza kujikwamua kiuchumi na sio vyama vyao vya kuweka na kukopa ambavyo wakati mwingine hujumuisha watu ambao si wanachama wa NSSF.

Akizungumza wakati wa kuutambulisha utaratibu huo kwa wafanyakazi wa Kamapuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Makao Makuu Tabata, Dar es Salaam jana, Meneja Mipango na Uwekezaji wa mfuko huo, Abdallah Mseli alisema mpango huo una lengo la kuhakikisha wanachama wao wanapata mikopo kwa riba nafuu.

Alisema utaratibu ulivyo ni kuwa wanachama hao kupitia Saccos zao wanajiorodhesha na kubainisha mahitaji yao ya mikopo kila mmoja na kuwasilisha maombi hayo NSSF ambao huyapitia na kuidhinisha fedha hizo kulingana na maombi ya wanachama kwa riba ambayo alisema ni ya chini sana kulinganisha na ile inayotolewa na benki. Mseli alisema benki nyingi zimekuwa zikitoza riba ya kati ya asilimia 18 hadi 25 kiwango ambacho kimekua kikidaiwa kuwa ni kikubwa na chini ya utaratibu huo wa NSSF, Saccos zitakuwa zinachukua asilimia tatu tu ya riba na mikopo inayotolewa na ni kwa ajili ya dharura, elimu na maendeleo.

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF, Crescentius Magori alisema kiasi ambacho kinatolewa kwa kila Saccos ni kuanzia Sh50 milioni hadi 1bilioni 1 na hadi sasa wameishatoa wastani wa Sh1.7bilioni kwa Saccos sita na wanachama 245 wa mfuko huo wamenufaika na mikopo hiyo.

“Zipo fedha za kutosha hivyo ni fursa yenu muhimu kuweza kujikwamua kiuchumi” alisema Magori na kuongeza kuwa pia mfuko huo unatoa huduma zingine ikiwa ni pamoja na mafao ya uzazi wanawake.

No comments:

Post a Comment