Serikali yakiri mafao ya wastaafu hayatoshi
16th February 2011
B-pepe
Chapa
Maoni
Serikali
imekiri kuwa mafao yanayotolewa hivi sasa na mifuko mbalimbali ya
hifadhi ya jamii nchini bado ni madogo kulinganisha na hali ya maisha.
Vile
vile, imesema imejipanga kuifanyia marekebisho makubwa mifuko hiyo ili
iweze kutoa mafao makubwa zaidi kwa wanachama wake tofauti na mafao
wanayoyapata sasa.
Hayo
yalisemwa jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano baina ya Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na
waandishi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Kamishna
Msaidizi wa Kazi (Hifadhi ya Jamii), Daudi Kaali, alisema mafao
yanayotolewa sasa ni duni mahitaji halisi ya wakati huu hivyo kuna haja
ya kufanya marekebisho.
Alisema
ingawa hali iko hivyo, baadhi ya mifuko imekuwa ikijitahidi kuongeza
mafao kila inapoona inafaa na alitoa mfano wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF), ambao hivi karibuni uliongeza mafano kwa wanachama wake
kutoka shilingi 52,000 kwa mwezi hadi 80,000.
Alisema baadhi ya mifuko mingine nayo imeongeza mafao hayo kutoka shilingi 21,000 hadi 40,000.
Kaali
alisema mamlaka ya SSRA kusimamia mabadiliko ya mifuko hiyo ili iweze
kutoa mafao manono yatakayowawezesha wastaafu kuishi maisha mazuri
zaidi.
Alisema
vile vile mifuko ya hifadhi ya jamii inawajibu wa kusaidia watu wa
makundi yasiyojiweza kama wanavyochangia katika maeneo mengine.
Naye
Mkurugenzi wa Mipangop na Utafiti wa SSRA, Ansgar Mushi alisema mafao
yanayotolewa yanapaswa kulingana na thamani ya pesa ya wakati uliopo.
Alisema
mifuko ya hifadhi ya jamii iwekeze kokote inakotaka lakini inatakiwa
mafao inayotoa yawe na maana kubwa kwa maisha ya wanachama wao.
Alisema
hivi sasa asilimia 3.5 tu ya watanzania ndio wako katika mifuko ya
hifadhi ya jamii na kwamba SSRA imejipanga angalau kuongeza idadi hiyo
hadi kufikia asilimia 20 kwa muda mfupi ujao.
“Tunapaswa
kutoka hapo tulipo kwenda hadi asilimia 20, twende 50 hadi asilimia 100
maana hifadhi ya jamii ni haki ya msingi na inahusu haki za binadamu,
kwa kuwa kuishi ni haki ya binadamu lazima vyombo vya umma kama SSRA
imwezeshe mtu kuishi maisha mazuri,” alisema.
Alisema
utafiti uliofanywa na Shirika la Kazi Duniani miaka michache iliyopita
unaonyesha kuwa asilimia 35 ya watu wanaofanyakazi hapa nchini ni
maskini na wanapostaafu wanaishi maisha ya shida.
Alisema mifuko ya hifadhi ya jamii iboreshwe ili iweze kutoa mafao ya kuwanufaisha wastaafu.
“SSRA
inawajibu wa kuhakikisha mfumo huu unawajumisha watanzania wengi na hata
mafao yanayotolewa yawe ya viwango vya kimataifa na watu wapate huduma
zinazolingana hivi sasa tofauti ya mafao ni kubwa sana baina ya makundi
katika jamii,” alisema.
Mwenyekiti
wa Bodi ya SSRA, Siraju kaboyonga alisema tatizo la ucheleweshaji wa
mafao katika mifuko ya jamii inasababishwa na ukosefu wa utunzaji mzuri
wa kumbukumbu.
Alisema
kuna wakati wanachama wamekuwa wakiulizwa barua za ajira zao kabla ya
kupata mafao yao jambo linalowawea gumu kwani wengi wao waliajiriwa
miaka mingi iliyopita.
“Mimi
niliajiriwa Benki Ku ya Tanzania (BoT), mwaka 1974 leo hii ukiniambia
nilete barua ya mwajiri wangu ndipo unipe mafao yangu utakuwa unanitesa
maana sina, utunzaji wa kumbukumbu ni changamoto kubwa katika utoaji wa
mafao ya wanachama,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment