Mifuko ya hifadhi ya jamii yaaswa kuboresha mafao ya wanachama
13th July 2011
B-pepe
Chapa
Maoni
Hifadhi ya jamii (NSSF)
Katibu wa Tughe mkoa wa Mara, Watson
Lushakuzi, alitoa kauli hiyo katika taarifa yake ya utekelezaji wa kazi
wa chama hicho katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
iliyowasilishwa kwenye mkutano mkuu wa Tughe mkoa.
Lushakuzi alisema mafao yanayotolewa kwa
watumishi wa mifuko hiyo ni kidogo sana jambo linalowafanya wastaafu
kuendelea kukabiliwa na hali ya umaskini licha ya kutumikia utumishi wao
kwa zaidi ya miaka 30.
Alitolea mfano wa watumishi wengi
waliostaafu miaka ya hivi karibuni wakiwa wamejiunga na mifuko hiyo
wamejikuta wakiambualia kiasi cha kati ya Sh. 700,000 na milioni 1.2
huku wenzao wa Mfuko wa Utumishi wa Umma (PSPF) wakivuna mamilioni ya
shilingi wanapostaafu.
Ameishauri mifuko hiyo ya NSSF, LAPF, PPF
na GEPF kuboresha huduma ya mifuko kwa wanachama wake kama ilivyofanyika
kwa Mfuko wa Watumishi wa Umma (PSPF) badala ya kuegemea zaidi kutumia
fedha za wanachama kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwemo ile ya
ujenzi wa majengo ya kibiashara, madaraja na vivuko.
Katibu huyo wa Tughe mkoani Mara ambaye
pia ni mwanachama wa NSSF, alisema licha ya makato yanayofanywa na
mifuko hiyo, bado huduma wanazotakiwa kupewa wanachama hazitolewi kabisa
ikiwa ni pamoja na matibabu, mafao ya ulemavu, huduma za mazishi huku
wastaafu wakikosa pesheni ya kila mwezi.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment