Pages

Tuesday, May 29, 2012

Dk Bilal: Mifuko ya hifadhi ya jamii ina mchango mkubwa

20th April 2012
Chapa
Maoni
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini imetajwa kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa sekta ya fedha ambayo imekua kwa zaidi ya asilimia 80 kwa kipindi cha miaka tisa kutoka Sh. bilioni 1,637 mwaka 2001 hadi Sh. bilioni 10,040 mwaka 2009.

Hayo yalisemwa jijini Mwanza jana na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF) unaofanyika jijini hapa.

Dk. Bilal alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ukiwemo GEPF katika kukuza uchumi wa taifa hususani sekta ya fedha.

Kwa mujibu wa Dk. Bilal, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inachangia asilimia 21 katika sekta ya fedha kiwango alichosema ni kikubwa.

Hata hivyo, alisema bado ni Watanzania wachache sana wanaopata kinga dhidi ya majanga kupitia mifuko hiyo.

Alifafanua kwamba takwimu zinaonyesha kuwa kati ya Watanzania milioni 22.4 wenye uwezo wa kuzalisha kipato, waliojiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii hawazidi asilimia sita.

Awali katika maelezo yake mafupi kwa mgeni rasmi, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya GEPF, Ladslaus Salema, alisema mpango wa hiari wa kujiwekea akiba ya uzeeni ulianzishwa na mfuko huo umekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka miwili cha utekezwaji wake.

Alisema tangu mwaka 2009 mpango huo ulipoanzishwa jumla ya Watanzania 11,219 wamejiunga na kujiwekea akiba ya Sh. milioni 994.07 hadi kufikia mwezi Machi, mwaka huu.


CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment