Pages

Saturday, February 4, 2023

RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA 20 WA WAKUU WA NCHI ZA EAC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wa Mkutano Maalum wa 20 wa Wakuu hao wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Bujumbura nchini Burundi tarehe 04 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Ikulu ya Bujumbura nchini Burundi kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalum wa 20 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tarehe 04 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Bujumbura nchini Burundi kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalum wa 20 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tarehe 04 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Bujumbura nchini Burundi kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tarehe 04 Februari, 2023.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa Wimbo wa Jumuiya hiyo ukipigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano Maalum wa 20 wa Wakuu hao wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Bujumbura nchini Burundi tarehe 04 Februari, 2023.







No comments:

Post a Comment