Pages

Sunday, November 6, 2022

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWATEMBELEA WALIONUSURIKA AJALI YA PRECISION AIR

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimfariji majeruhi Levina Theonest Lutinda na mtoto wake Emmily Victor katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambao wameokolewa katika ajali ya ndege iliyotolea leo asubuhi mkoani Kagera.

NA OWM, BUKOBA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Kagera kushuhudia zoezi la uokoaji wa Ndege ya Shirika la Precision Air iliyopata ajali katika Ziwa Victoria, Bukoba mkoani Kageriliyopata ajali mkoani Kagera.

Majaliwa amewajulia hali wahanga wa ajali wanaopata matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Kagera.

Majaliwa akizungumza katika eneo hilo amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa watu wote walioguswa na ajali hiyo na kwamba Serikali itaendelea kutoa huduma stahiki kwa majeruhi wote.

Pia amewataka wananchi kuwa na subra katika kipindi hiki ambacho Serikali itafanya uchunguzi kupitia vyombo vyake ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Issessanda Kaniki amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 19. Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimfariji majeruhi Levina Theonest Lutinda na mtoto wake Emmily Victor katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambao wameokolewa katika ajali ya ndege iliyotolea leo asubuhi mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment