Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax wa tatu kutoka kulia wakizundua mfumo wa taarifa kwa wawekezeji, mfumo umezinduliwa leo Novemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mfumo wa taarifa kwa wawekezeji, mfumo umezinduliwa leo Novemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uwezaji, Exaud Kigahe akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa taarifa kwa wawekezeji, mfumo umezinduliwa leo Novemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wizara ya Viwanda, Uwekezaji na Biashara, Ally Gugu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa taarifa kwa wawekezeji, mfumo umezinduliwa leo Novemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa masuala ya Uwekezaji, SDGs kutoka UNDP, Joanne akifafanua namna walivyoshauriana kuanzisha Mfum wa Taarifa kwaajili ya mwekezaji wa ndni na nje ya nchi katika wa uzinduzi wa mfumo wa taarifa kwa wawekezeji, mfumo umezinduliwa leo Novemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa shirika la UNDP, Christine Musisi, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mfumo wa taarifa kwa wawekezeji, mfumo umezinduliwa leo Novemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam.
Picha za Pamoja.
Baadhi ya wadau wa uwekezaji wakiwa katika uzinduzi wa mfumo wa taarifa kwa wawekezeji, mfumo umezinduliwa leo Novemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam.
SERIKALI imetaja vipaumbele katika uwekezaji ambavyo ni Kilimo, Usalama wa Chakula, Nishati (Nishati jadidifu), Elimu, Utalii na Miundombinu.
Vipaumbele hivyo vimeainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa katika Uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki jijini Dar es Salaam leo Novemba 30, 2022. Amesema kuwa Mfumo huo utawawezesha wawekezaji wa ndani na nje nchi kupata taarifa za fursa mbalimbali na masoko.
"Lengo la kuzindua Mfumo wa taarifa kwa mwekezeji ni kuweka bayana Masoko na fursa na taarifa zote ambazo zinahitajika katika uwekezaji mwekezaji aweze kuwekeza nchini ili kuleta maendeleo katika taifa letu." Amesema Tax
Dkt. Tax amesema kuwa katika jukwaa hilo limelenga kuweka njia ya mabadilishano ya mawazo kuhusu sera ya taifa ya ajenda ya Tanzania kuhamasisha uwekezaji wa Malengo ya maendeleo endelevu na kurahisisha maendeleo ya nchini.
Pia majadiliano ya utoaji mitaji ya ndani na kimataifa chini ya mfumo wa SDGs ulijadiliwa ukiwa na madhumuni ya uwekezaji katika biashara na uwekezaji baina yawawekezaji na wafanyabiashara wanaowezesha uelewa wa taarifa za masoko ya bidhaa mbalimbali.
Kwa Upande wa Naibu Waziri wa Uwezaji, Exaud Kigahe amesema kuwa Changamoto iliyokuwepo ni kukosa kwa taarifa za uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, amesema sasa mfumo huo utaonesha fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kwa mataifa mengine duniani.
Kigahe amesema hakuna masharti yeyote katika uwekezaji ni kuwa na vifaa vya teknolojia ya kisasa ili kuweza kuingia katika Mfumo huo kwa kuweza kupata taarifa za sekta unayotaka kuwekeza au kufanya biashara.
"Serikali inapoendelea kutengeneza mazingira wezeshi kwa wawekezaji, Watanzania wachangamkie fursa hiyo kwani uwekezaji sio kwa watu wa nje ya nchi tuu bali ni ya Watanzania wote.
Kigahe amesema serikali ya awamu ya sita inahuisha sera zote zilizo katika sekta ya uwekezaji, hasa katika sera ya biashara, Uwekezaji na sera ya viwanda ili kuziwekea mikakati mipya ambayo inaendana na maboresho ya mifumo mbalimbali ya kiteknolojia.
Amesema kuhuisha sera hizo pia wameweza kupunguza masharti magumu katika uwekezaji ambayo yalikuwepo kabla ya kuziangalia upya sera hizo ili kuwezesha hata mwenye mtaji mdogo kuweza kuvutiwa na uwekezaji.
Akielezea namna wanavyoshirikiana na Serikali Mwakilishi Mkazi wa shirika la UNDP, Chritine Musisi amesema kuwa UNDP inashirikiana na Serikali katika kutengeneza mfumo wa taarifa za uwekezaji zitakazo mwezesha mwekezaji kupata taarifa na fursa za uwekezaji zilizopo pamoja na masoko kwa wawekezaji wa ndani ya nchi na nje ya nchi ili kuleta maendeleo nchini.
"Tanzania inafursa nyingi katika sekta ya Miundombinu, Utalii, Kilimo, Uhifadhi wa chakula, Elimu na Nishati. Amesema Musisi
Jukwaa hilo ni la kwanza kwa Tanzania la uwekezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) limeratibiwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara(MIIT) na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF)
No comments:
Post a Comment