Arusha. Msiba wa watoto wawili wa wafanyabiashara marufuku jijini la Arusha, waliokuwa wachumba umeibua simanzi na kutawaliwa na usiri kuhusu chanzo cha ajali iliyosababisha vifo vyao.
Watoto hao, Estomi Temu na mpenzi wake, Nice Mawala (24), Mkazi wa Njiro wamefariki dunia kwa ajali mbaya eneo la Kwa Mrefu jijini humo juzi majira ya saa 7:30 usiku walidaiwa kutoka klabu ya starehe.
Vivyo hivyo tangu kutokea ajali hiyo sio, kamanda wa Polisi, Justin Masejo wala ndugu ambao wamekuwa tayari kutoa taarifa za tukio hilo.
Kamanda Masejo tangu juzi kupitia msaidizi wake, waliahidi kutoa taarifa za ajali hiyo lakini hadi jana Jumapili, Julai 31, 2022 licha ya kukiri kuna taarifa za ajali hiyo.
"Bado taarifa rasmi inaandaliwa kuhusiana na hilo na ikiwa tayari itatolewa huenda kesho (leo) Jumatatu," alisema mmoja wa wasaidizi wa Kamanda Masejo jina linahifadhiwa.
Kwa upande wa ndugu katika msiba huo, pia wamegoma kutoa taarifa na wanahabari wamezuiwa kuingia kwenye msiba eneo la kwa mrefu wa alipokuwa anaishi marehemu Nice.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Jonathan Peter amesema ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 7:30 usiku katika eneo hilo wakati gari aina ya Range Rover walilokuwa wakitumia lilikuwa kwenye mwendo kasi na kuanguka.
"Baada ya ajali ule usiku, polisi walifika na kuwachukuwa wale vijana na baadaye tulielezwa wamefariki," alisema Peter.
Miili ya wachumba bado imehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Mkoa Arusha ya Mount Meru.
No comments:
Post a Comment