Pages

Thursday, July 21, 2022

Tunakwenda Kutoa Elimu Ya Suala La Katiba Kwa Wananchi -Dkt.Ndumbaro

Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana vipaumbele vya Wizara hiyo kwa mwaka fedha 2022/2023 jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kubuda, Michuzi Tv
WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro amesema kipaumbele cha wizara yake katika mwaka huu wa fedha tunakwenda kutoa elimu kwa Wananchi suala ya Katiba.

Ndumbaro ameyasema hayo jiji Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumza na namna ya Wizara hiyo ilivyojipanga kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutoa elimu suala la katiba.

Ndumbaro amesema kuwa katiba inazungumzwa na wanasiasa hivyo wadau muhimu wa katiba ni wananchi ambao wanatakiwa kusikilizwa.

Amesema kuwa katika kwenda na katiba watashirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia kutoa elimu ili jambo liwe shirikishi.

Aidha amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM)kupitia Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu ameonyesha njia juu suala la katiba.

"Lengo letu ni kuwasaidia Wananchi kuwa na uelewa
mpana wa katiba na umuhimu wake katika kupata haki zao kutokana na maoni yao kwenye katiba" amesema Dkt.Ndumbaro

Ndumbaro amesema kuwa kwa mwaka huu wa fedha wanakwenda kufanya maboresho kwenye vyombo vya kutoa haki ikiwemo mahakama kwa kijenga mahakama tisa.

Amesema kuwa maboresho ya mahakama ni katika kutoa haki kwa wananchi kwa wakati kwani kwani haki inayocheleweshwa ni haki iliyodhulumiwa.

Katika hatua nyingine wanakwenda kuangalia makosa yasiyo na dhamana kuweza kupata dhamana kutokana na sheria ambazo zitawekwa.

Dk.Ndumbaro amesema katika maboresho mengine na Chuo cha Mahakama Lushoto na Shule ya Sheria kumekuwa na maoni mbalimbali ya wadau.

Amesema vipaumbele vingine vya Wizara hiyo ni pamoja na kutekeleza mpango wa kutumia Lugha ya Kiswahili katika utoaji wa haki nchini ambapo hadi sheria 220 zimeshatafsiliwa kutoka lugha ya kiingereza.

No comments:

Post a Comment