Pages

Saturday, July 30, 2022

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA 65 WA UNWTO KWA KANDA YA AFRIKA


JAMHURI ya Muungano wa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Shirika la Utalii Duniani ( UNWTO), utakaofanyika mjini Arusha kuanzia tarehe 5 - 7 Oktoba 2022.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Paris  kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii ulikuwa mstari wa mbele kuzishawishi nchi wanachama wa UNWTO kukubali mkutano huo ufanyike  nchini Tanzania.

 Mkutano huo pamoja na kuwaleta Mawaziri wa Utalii kutoka nchi zote za Afrika, pia utahudhuriwa na wadau wa utalii kutoka nchi mbali mbali duniani wanachama wa UNWTO.

 Aidha, Mkutano huo utaitangaza zaidi filamu ya Tanzania Royal Tour yenye lengo  la kukuza sekta ya Utalii na kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo. Juhudi hizo ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kujikita katika utalii wa mikutano.

No comments:

Post a Comment