Dar es Salaam. Siku tatu baada ya Dk Raphael Chegeni, kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, uteuzi wake umetenguliwa.
Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Julai 31, 2022 saa 1 usiku na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imesema Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi huo na kumteua Meja Jenerali Suleiman Mzee kuchukua nafasi hiyo.
Rais Samia alimteua Dk Raphael Chegeni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Julai 28, 2022 kuchukua nafasi ya Ally Hapi.
Katika taarifa ya Ikulu imesema mkuu huyo wa nchi amemtengua uteuzi wa Dk Chegeni huku nafasi hiyo ikichukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Jenerali Suleiman Mzee.
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali Suleiman Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na kutengua uteuzi wa Dk Raphael Masunga Chegeni” imesema taarifa hiyo
Taarifa hiyo imesema kuwa uapisho wa mkuu huyo wa mkoa utafanyika kesho Ikulu ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment