Mwanafunzi wa Chuo cha VETA cha Mafunzo ya
Hoteli na Utalii (VHTTI) kilichopo Njiro mkoani
Arusha Happiness Michael akiwa ameshika ndizi
Kitarasa ambayo ikichanganywa na mbaazi
inatengeza vyakula ambavyo vinatibu magongwa
mbalimbali yakiwemo ya sukari, pasha , kuongeza
kinga ya mwili pamoja na kuimarisha afya ya akili
kwa mtoto.Mwanfunzi huyo yuko kwenye banda la
VETA katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya
Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya
Sabasaba mkoani Dar es Salaam.
Happiness Michael ambaye ni mwanafunzi wa
Chuo cha VETA ch Mafunzo ya Hoteli na Utalii
kilichopo Njiro mkoani Arusha akionesha unga
unatokana na ndizi kitarasa ambayo inatumika
kutengeneza aina mbalimbali za vyakula.
Baadhi ya wanafunzi na walimu wa Chuo cha
VETA cha Mafunzo ya Hoteli na Utalii Njiro mkoani
Arusha wakiwa katika picha ya pamoja kwenye
kwenye banda la VETA.
Na Said Mwishehe, Michuzi TVCHUO cha VETA cha Mafunzo ya Hoteli na Utalii(VHTTI) kilichopo Njiro mkoani Arushaambacho kinamilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)kimekuja na ubunifu wa mazao ya ndizi kitarasa na mbaazi kutengezavyakula ambavyo vinatumika kutengeneza vyakulaambavyo ni tiba ya kutibu magonjwa mbalimbaliyakiwemo ya kisukari na presha.Akizungumza kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa
ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya MwalimuNyerere maarufu Sabasaba Mwanafunzi
anayesomea katika
chuo hicho Happiness Michaelamesema kwa mwaka huu katika maonesho hayo
wamekuja na ubunifu wa mapishi kwa kutumia ndizi
kitarasa na mbaazi.
“Sisi na walimu wetu katika maonesho ya mwaka
huu tumekuja na ubunifu wa mazao ambayo ni ndizi
na mbaazi na ndizi , hii ndizi ambayo tumeileta hapa
iko tofauti na ndizi zingine, hivyo tumeamua
kuchagua ndizi Kitarasa na mbaazi ni kwasababu
mazao hayo yalikuwa hayapewi kipaumbele katika
mlo wa binadamu.
“Kwa hiyo sisi tumechukua hiyo fursa na tulilenga
kwa watu ambao hawatumii ngano kwa hiyo
tumetumia ndizi kitarasa pamoja na mbaazi
kutengeza baadhi ya vyakula ama vyakula vyote
vinavyokuwa vinatengenezwa na ngano, mfano
mkate , maandazi ,biskuti, keki na hiyo sio moja kwa
moja mtu anakula tu lakini anakuwa anapata
tiba.Mtu anapotumia ndizi kitarasa na mbaazi
anakuwa anatibu kisukari , presha, mwili wenye
kujaa mafuta na vile vile kwa wale
wanaosumbuliwa na tatizo la kinga za mwili
zinakuwa zinashuka.
“Na hata watoto zinakwenda kujenga afya ya akili,
ndizi ya kitasara yenyewe iko tofauti na ndizi
nyingine na yenyewe kinachoangaliwa ni ule
utomvu ambao ndio tiba yenyewe na ndio maana
tukaamua kuchagua ndizi kitarasa.Hata wanaotaka
kuacha kuvuta sigara ni vema wakatumia ndizi
kitarasa na mbaazi .
“Hii ndizi unaweza kutumia ikiwa mbivu, ikipikwa ,
na unga, lakini kwa sisi tulikuwa tunalenga kutumia
unga , hivyo tulikuwa tunachukua ndizi kitarasa
kisha tunamenya tunaanika na tukishaanika
tunakwenda kusaga na kupata unga kwa ajili ya
matumizi ya kutengeza vile vitafunwa.Hii ndizi na
tangu enzi na enzi na kule Kilimanjaro zamani
ilikuwa inatumika wakati wa njaa,”amesema.
Wakati huo huo, amesema chuo chao mbali ya kuja
na ubunifu wa mazao hayo ,wamekuw wakielezea
kozi ambazo zinafundishwa katika chuo chao
ambacho kipo kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota
tatu.Ametaja baadhi ya kozi ni uokaji mikate, keki
na mapishi ya vyakula, mapambo na upambaji wa
kumbi za starehe, mafunzo ya kompyuta na mbinu
za uandaaji Cocktail.
Kozi nyingine ni ya usafi wa majengo na maeneo ya
wazi, huduma kwa wateja , mbinu za ujasiriamali,
usimamizi wa shughuli za mapokezi na vyumba,
uhudumu na uuzaji wa chakula na vinywaji,
uaandaji na upishi wa chakula , utaalamu wa
uongozaji watalii pamoja na uandaaji na uendeshaji
wa safari za watalii.
No comments:
Post a Comment