Pages

Wednesday, June 1, 2022

Ubalozi Wa Uingereza Kusherehekea Miaka 70 Ya Utawala Wa Malikia Elizabeth II Na Miaka 60 Ya Urafiki Wa Tanzania Na Uingereza


UBALOZI wa Uingereza nchini Tanzania uliopo jijini Dar es Salaam itasherekea Siku ya Kuzaliwa ya Malikia Elizabeth II wa Uingereza Juni, 2 2022 pamoja na wageni waalikwa kuwa Viongozi wa Serikali, Jumuiya ya Diplomasia nchini, Mashirikia yasiyo kuwa ya Kiserikali, Sanaa, na Umoja wa Waingereza Tanzania.

Sherehe za mwaka huu zina umuhimu wa kipekee kwani Uingereza inaadhimisha miaka 96 ya Malikia Elizabeth na Jubilei ya miaka 70 ya Utawala wake. Malikia ametawala kwa muda mrefu zaidi kuliko mfalme mwingine yeyote katika historia ya Uingereza.

Siku ya kuzaliwa ya Malikia ni wakati muhimu wa kusherehekea urafiki kati ya Tanzania na Uingereza ambao mwaka huu inatimiza miaka 61 ya ushirikiano baada ya uhuru.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberata Mulamula.

Kabla ya hafla hiyo, David Concar, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, alisema:

"Huu ni wakati maalum. Tunasherehekea miaka 70 ya utawala wa Malikia na kujitolea kwake kwa Uingereza na Jumuiya ya Madola. Pia tutasherehekea miongo sita ya urafiki ya baada ya uhuru kati ya Uingereza na Tanzania na kuashiria mustakabali mzuri wa uhusiano huu wa kudumu kati ya nchi hizi mbili za Jumuiya ya Madola.

Katika sherehe hizi, Mwangaza wa Jubilei utawashwa tarehe 2 Juni 2022, Bagamoyo na Moshi kama mojawapo ya vinara 1500 vitakavyomulika kote Uingereza na Jumuiya ya Madola kama ishara ya umoja katika kusherehekea Jubilei ya miaka 70.

Kuelekea siku ya kuzaliwa kwa Malikia and Jubilei, ‘Wiki ya Waingereza’ (British Week) imefanyika hapa Dar es Salaam ikileta waingereza pamoja katika sanaa, michezo na biashara.

Nchini Uingereza, watu watasherehekea Jubilei kwa siku nne kuanzia Ijumaa na kuwa na programu pana ya matukio ya umma ikijumuisha gwaride la Siku ya Kuzaliwa, Ibada ya Shukrani na tamasha kuu la umma katika Jumba la Buckingham.

No comments:

Post a Comment