Pages

Sunday, June 5, 2022

SBL Kuwawezesha Vijana Kushiriki Kwenye Sekta Ya Kilimo

 

Makamu mkuu wa chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani Maximillian Sarakikya (wa tatu kulia) akiwaeleza kitu baadhi ya wafanyakazi kampuni ya bia ya Serengeti waliotembelea chuo hicho mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha ni wanafunzi wa chuo hicho ambao ni wanufaika na programu ya ufadhili wa masomo inayojulikana kama Kilimo Viwanda.

Wanafunzi wa chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani ambao ni wanufaika wa programu ya ufadhili wa masomo inayojulikana kama Kilimo Viwanda inayotolewa na kampuni ya bia ya Serengei wakiwa na furaha muda mfupi baada ya kupewa vyeti vyao vya kuchaguliwa kupata ufadhili .
Fredy Kogani, mfanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) akimkabidhi cheti Juma Khamisi, mwanafunzi wa chuo cha kilimo na mifugo cha Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo Pwani baada ya kuchaguliwa katika programu ya ufadhili wa masomo inayojulikana kama Kilimo Viwanda. Wa kwanza kushoto ni Maxmilian Sarakikya, makamu mkuu wa chuo hicho akifuatiwa na John Wanyancha, mkurugenzi wa mawasiliano kwa umma na mratibu wa masomo wa chuo hicho Chonge Mazengo

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imesema itaendelea kuwawezesha vijana ili waweze kuwa na ushiriki mpana zaidi katika kilimo.
Akiongea wakati wa kukabidhi vyeti kwa wanafunzi 27 wanaofadhiliwa na kampuni hiyo chini ya programu ya Kilimo Viwanda katika chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole, mkurugenzi wa mahusiano kwa umma wa SBL John Wanyancha alisema SBL inatambua umuhimu wa vijana kushiriki katika kilimo
“Vijana ambao tunawafadhili chini ya programu ya Kilimo viwanda, watakwenda kuongeza nguvu kwenye sekta hii muhimu kwa uchumi wa nchi yetu. Mchango wao utakuwa muhimu sana katika kuhakikisha kilimo chetu kinakuwa na tija,” alisema.
Wanyancha alisema SBL hutumia malighafi zinazotokana na kilimo kutengenezea bia zake ikiwa ni Pamoja na shayiri, mtama na mahindi na kuongeza kuwa uwepo wa wataalamu wa kutosha utasaidia upatikanaji wa malighafi hizo ambazo mahitaji yamekuwa yakiongezeka
“Mahitaji yetu ya malighafi yanaongezeka kila mwaka. Mwaka 2021 kwa mfano tulinunua tani 18 za malighafi ambazo ni saw ana asilimai 80 ya mahitaji yetu kwa mwaka. Lengo letu ni kufikia asilimia 85 ifikapo mwaka 2025,” alieleza
Kupitia programu ya kilimo Viwanda, SBL tayari imeshatoa ufadhili kwa wanafuzi zaidi ya 200 wanasomea masomo ya kilimo katika vyuo vinne ikiwa Pamoja na Kaole cha Bagamoyo, Kilacha cha Moshi Mt. Maria Goretti cha Iringa na Igabiro kilichopo Muleba mkoani Kagera..
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Kaole Sinani Simba aliishukuru SBL kwa kutoa ufadhili kwa wanafunzi ambao amesema pasipo msaada huo wengi wao wangeshindwa kumaliza masomo yao kutokana na changamoto ya kushindwa kulipa ada.
“Mchango wa SBL siyo tu unawasaidia wanafunzi wanaotoka katika familia duni kupata fursa ya kuendelea na masomo, bali pia unasaidia kukuza sekta ya kilimo hapa nchini kupitia kuongeza wataalamu ambao takwimu zinaonyesha ni wachache ukilinganisaha na mahitaji,” alisema.

No comments:

Post a Comment