Pages

Tuesday, May 31, 2022

Serikali Yawaunga Mkono TBL Na Vodacom Katika Jitihada Za Kuinua Kilimo


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, akizungumza waandishi wa habariDar es Salaama jana baada ya kuzindua Mfumo wa mtandao wa malipo kwa wakulima unaojulikana kama ‘BanQu’ wa Kampuni ya TBL na Vodacom Tanzania Plc kupitia M-Pesa, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Sitholizwe Mdlalose na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Jose Moran.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa mtandao wa malipo kwa wakulima unaojulikana kama ‘BanQu’ wa Kampuni ya TBL na Vodacom Tanzania Plc kupitia M-Pesa, Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye(wa tatu kushoto) akiwa na Wakurugenzi wa Makampuni ya TBL na Vodacom Tanzania Plc wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa mtandao wa malipo kwa wakulima unaojulikana kama ‘BanQu’ , Dar es Salaam jana
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Sitholizwe Mdlalose, akifafanua jambo wakati wa kuzindua Mfumo wa mtandao wa malipo kwa wakulima unaojulikana kama ‘BanQu’ wa Kampuni ya TBL na Vodacom Tanzania Plc kupitia M-Pesa, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Jose Moran akielezea jambo wakati wa kuzindua Mfumo wa mtandao wa malipo kwa wakulima unaojulikana kama ‘BanQu’ wa Kampuni ya TBL na Vodacom Tanzania Plc kupitia M-Pesa, Dar es Salaam leo Mei 31, 2022 jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV

SERIKALI inaunga mkono jitihada za Kampuni ya Vinywaji vikali ya TBL na Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania kwa kunyanyua uchumi kupitia kilimo kwa kutengeza mfumo wezeshi kwa wakulima kwenye kulifikia soko .

Waziri Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hayo leo Mei 31, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mfumo wa malipo kwa wakulima uliopewa jina la BanQu unaofanywa na Vodacom pamoja ma TBL.

Amesema, Serikali inapongeza na kuunga mkono jitihada hizo zitakazoinua sekta ya kilimo.

"Nichukue nafasi hii kuwapongeza wenzetu wa Vodacom na TBL kwa kuzindua mfumo huu utakaostawisha sekta ya kilimo na wakulima , sekta hii inagusa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na baadaye taifa zima na ndio sekta inayowashughulisha watanzania asilimia 70 mpaka 80" amesema Nape.

Nape amesema, Vodacom kupitia M-Pesa imerahisisha mfumo wa kifedha kwa wakulima kwa kuwa huduma za benki hazipo vijijini ambapo wakulima hupatikana.

Uamuzi wa Vodacom unakwenda kuwasaidia wakulima kwenye huduma za kifedha na kutasaidia uchumi wa nchini yetu" amesema Nape.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Jose Moran amesema kuwa Teknolojia ya BanQu itawezesha wakulima kupata taarifa zitakazo wawezesha kulinda maslahi ya wakulima.

Morani amesema kuwa TBL imeweka mipango thabiti ya kuwanufaisha wakulima "Hivi sasa asilimia 74 ya malighafi inayotumiwa na TBL inatoka kwa wakulima wa ndani ya nchi".

Naye, Mesia Mwangoka Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TBL amesema kuwa mfumo huo tayari ushasajili zaidi ya wakulima 6500 wanaouzia mazao kupitia TBL na watalipwa kupitia M-Pesa, ambayo itaongeza mnyororo wa thamani.

"Kupitia Mfumo wa BanQu shughuli zote za manunuzi na malipo kati ya TBL na wakulima zitawekwa kwenye kumbukumbu ili kuwezesha ufuatiliaji na uhakiki kwa pande zote mbili kwa njia ya kidigitali.

Mkuregenzi Mkuu wa Vodacom Sitholizwe Mdlalose amesema kuwa Vodacom kupitia mfumo wa BanQu imekusudia kuwainua wakulima na kuwapatia tija wakiwa huko huko mashambani bila kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za kifedha.

Amesema huduma hiyo itaongeza thamani ya mazao yao kwa kuwa inapunguza mianya ya upotevu wa pesa unaotokana na kusubiri kwa muda mrefu au kutembea umbali mrefu kwa ajili kufuatilia malipo yao.

Naye Epimack Mbeteni Mkurugenzi wa M-Pesa amesema kuwa Vodacom ikishirikiana na TBL imeamua kurahisisha huduma za kifedha kwa wakulima ambao awali walikuwa wakipata changamoto kutokana na kuwa mbali na hudama za kifedha.

Mbeteni amesema kuwa Vodacom inakwenda kuwakomboa Watanzania kwa kuwa mtandao huo imejidhatiti kwenye kuwahudumia wananchi.

"tumezindua huduma ya Bima ambayo kuna Bima ya Afya, Bima ya Kilimo zitakazokwenda kuwasaidia wakulima kwenye shughuli zao " amesema Mbeteni.

No comments:

Post a Comment