Pages

Saturday, April 2, 2022

TRA YAENDELEA KUVUNJA REKODI YA MAKUSANYO YA KODI

Kamishna Mkuu TRA, Bw. Alfayo J. Kidata.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imevunja rekodi yake ya ukusanyaji mapato ambapo KATIKA kipindi cha Robo Tatu yaani

mwezi Julai hadi Machi kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 imekusanya Shilingi Trilioni 16.69 ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.3 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 17.15.

Taarifa iliyotolewa na TRA na kusainiwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Alfayo J. Kidata, mapema Leo asubuhi Aprili 3, 2022 imesema makusanyo hayo ni ongezeko la Shilingi Trilioni 3.1 ukilinganisha na kiwango Cha makusanyo ya Shilingi Trilioni 13.59 kilichokusanywa katika kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021.

“Ongezeko hili ni ukuaji wa makusanyo WA asilimia 22.8.” Taarifa hiyo imesema.

Taarifa kamili hii hapa.





No comments:

Post a Comment