Pages

Thursday, April 28, 2022

Sh950 milioni zatengwa kuboresha miundombinu

nyasapiic

By Sharon Sauwa

Dodoma. Serikali imesema Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) imetenga

Sh950 milioni za kuboresha miundombinu ya mitaa ya viwanda.

Akijibu swali leo Alhamisi Aprili 28, 2022 la Mbunge wa Nyasa (CCM), aliyehoji ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa kituo cha Sido wilayani Nyasa, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema katika bajeti ya mwaka 2022/23 wizara hiyo kupitia Sido imetenga Sh950 milioni za kuboresha miundombinu ya mitaa ya viwanda.

Amesema kati ya fedha hizo, Sh100 milioni ni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha mafunzo na uzalishaji cha Sido wilayani humo.

 “Hivyo, pindi fedha hizo zitakapopokelewa, ujenzi wa kituo hicho utakamilika,”amesema.

No comments:

Post a Comment