Pages

Wednesday, April 27, 2022

PSSSF YAPONGEZA JITIHADA ZA RAIS SAMIA KUIFUNGUA NCHI, WAPANGAJI KWENYE MAJENGO YAKE YA VITEGA UCHUMI WAONGEZEKA

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), C.P.A Hosea Kashimba (kulia) na  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MIC Tanzania PLC, C.P.A  Innocent Rwetabura wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba utakaoiwezesha kampuni hiyo inayomiliki mtandao wa simu, Tigo kupangisha kwenye jengo la PSSSF Commercial Complex.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), C.P.A Hosea Kashimba (kulia) na  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MIC Tanzania PLC, C.P.A  Innocent Rwetabura wakisaini mkataba wa pango chini ya uangalizi wa wanasheria wa taasisi hizo mbili.
Jengo la kisasa la kitegauchumi la PSSSF Commercial Complex lililoko barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam. Pamoja na taasisi nyingine kubwa jengo hili ndio itakuwa makao makuu ya Kampuni ya MIC Tanzania PLC wanaomiliki mitandao ya simu ya Tigo na Zantel.
Jengo la kisasa la kitegauchumi la PSSSF Commercial Complex lililoko barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam. Pamoja na taasisi nyingine kubwa jengo hili ndio itakuwa makao makuu ya Kampuni ya MIC Tanzania PLC wanaomiliki mitandao ya simu ya Tigo na Zantel.

Moja ya kumbi za mikutano ndani ya jengo hilo
Bwawa la kuogelea kwenye jengo hilo
C.P.A Hosea Kashimba akizungumza wakati wa hafla hiyo.
C.P.A  Innocent Rwetabura, akizungumza kwenye hafla hiyo.
C.P.A Hosea Kashimba akiongozana na kutoka kulia, Mhandisi Marco Kapinga kutoka PSSSF, Fatma Elhady na Coletha Mnyamani wote kutoka Idara ya Uhusiano na Elimu kwa Umma, PSSSF, wakitembela jengo hilo.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF, James Mlowe (kulia), akibadilishana mawazo na  Sultan Mndeme, Mwenyekiti Mtendaji wa GIMCOAFRICA Limited, wanaosimamia jengo kwa niaba ya PSSSF.
C.P.A Hosea Kashimba akiwa na Sultan Mndeme, Mwenyekiti Mtendaji wa GIMCOAFRICA Limited, wanaosimamia jengo kwa niapa ya PSSSF


Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, C.P.A Hosea Kashimba (watatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MIC Tanzania PLC, C.P.A  Innocent Rwetabura (wapili kushoto), Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, PSSSF, James Mlowe (wakwanza kulia) na Meneja Uhusiano Tigo, Woinde Shisael wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha ya pamoja

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), C.P.A Hosea Kashimba amesema kuongezeka kwa idadi ya wapangaji kwenye

jengo jipya na la kisasa la Kitega Uchumi la PSSSF Commercial Complex lililoko barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam, ni matokeo ya jitihada kubwa anazofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan za kufungua nchi pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kufanya kibiashara.

C.P.A Kashimba ameyasema hayo Aprili 27, 2022 wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa upangishaji kwenye jengo hilo kati ya Mfuko na Kampuni ya MIC Tanzania PLC wamiliki wa Mtandao wa simu, Tigo katika hafla iliyofanyika kwenye jengo hilo.

“Kampuni ya Tigo kuamua kuyaweka Makao yake Makuu hapa ni heshima kubwa sana kwetu, lakini pia idadi ya wapangaji kwenye jengo letu imeongezeka na hivi karibuni tunategemea nafasi nyingi zaidi za jengo kujazwa kwakuwa tumeshasaini mikataba ya upangishaji na taasisi kadhaa kubwa, yote haya ni matokeo ya jitihada hizo za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.” Alisisitiza na kuongeza……. Ni matarajio yetu kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka huu hali ya upangishaji (occupancy rate) itakuwa imefikia zaidi ya asilimia 50% na hivyo kutimia kwa dhamira na malengo ya uwekezaji.

“Hali hii inauhakikishia Mfuko upatikanaji wa mapato na kuwezesha kurudisha gharama za uwekezaji na kuanza kupata faida ili kuwezesha kulipa Mafao kwa Wanachama wetu,” alisema.

Akichambua mandhari ya jengo hilo linalozungukwa na maeneo mashuhuri kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza, Mlimani City na Ubungo, C.P.A Kashimba alisema kuna Jengo la “executive” lenye ghorofa 14 mahsusi kwa ajili ya maofisi,  ukumbi wa shughuli za kibenki na ukumbi wa mikutano uliopo ghorofa ya 13 huku Jengo la biashara lenye ghorofa 35 ambalo linafaa kwa ofisi za ukubwa wa kuanzia mita za mraba 30 na kuendelea kulingana na utashi wa mpangaji.

Aidha kuna Jengo la ghorofa 3 la kumbi za mikutano zenye kumbi zenye uwezo wa kuchukua watu 15 hadi 900 kwa wakati mmoja pamoja na vyumba vya kupumzikia wageni mashuhuri (VIP);

“Kwa kuzingatia ukubwa wa Jengo lenyewe na ili kukidhi mahitaji ya wapangaji wetu kuna eneo la maegesho ya magari lenye ghorofa 6 lenye uwezo wa kuegesha magari zaidi ya 837 kwa wakati mmoja pamoja na eneo la mgahawa, bwawa la kuogelea, mazoezi ya Gym na burudani lililoko ghorofa ya 5.

Mbali ya sifa ya kuwa miongoni mwa majengo marefu na kubwa katika ukanda wa  Afrika Mashariki na Kati na kuwa kivutio; Mkurugenzi Mkuu alisema, PSSSF Commercial Complex ni jengo la kisasa lenye sifa na huduma zote muhimu kuendana na mahitaji ya wapangaji wetu.

Alisema Jengo hilo limejengwa kwa viwango vya kimataifa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya ujenzi inayozingatia utunzaji wa mazingira na kudhibiti matumizi ya nishati ya umeme.

“Kutokana na dhana ya kuwa “eco-friendly”; vioo vya madirisha vya jengo hili vina uwezo wa kuhifadhi baridi ya kiyoyozi isitoke nje, vivyo hivyo vinazuia joto la nje lisiingie ndani ya jengo na hivyo kubana matumizi ya nishati inayohitajika kuweka mfumo unaofaa wa hali ya hewa.” Alifafanua C.P.A Kashimba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MIC Tnazania PLC, C.P.A  Innocent Rwetabura, alisema kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa hivi karibuni na muungano wa Kampuni  ya Madagascar, Axian Group (Axian Telecom)na  Mfanyabiashara mkubwa hapa nchini Rostam Aziz  kuhusu kukamilika kwa mchakato wa ummiliki wa kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania PLC yaani Tigo na Zantel tunategemea ukuaji mkubwa unaopelekea uhitaji wa nafasi kubwa na tumeona sehemu sahihi kuhamia ni PSSSF Commercial Complex.

“Tunatarajia kuanza kuhamia hapa mwishoni mwa mwaka huu baada ya kukamilisha uwekaji wa miundombinu yetu itakayotuwezesha kufanya shughuli zetu na hivyo kutoa huduma z ahali ya juu kwa wateja wetu.” Alisema C.P.A Rwetabura.

No comments:

Post a Comment