Janeth Raphael - Dodoma
Serikali Imesema imetatua migogoro 18 kati ya 25 iliyopo.
Selemani Jafo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira, ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Muunganano wa Tanganyika na Zanzibar wamefanikiwa yaliyofanyika Kitaifa jijini Dodoma.
Waziri Jafo amesema kuwa mwaka 2020 waliweza kutatua kero saba na kubaki kero 18 za muungano.
“Lakini kwa uongozi wenu wewe (Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango) na mheshimiwa Rais (Rais Samia Suluhu Hassan) tumefanikiwa kutatua kero 11 (mwaka 2021) na hivyo ukijumlisha na zile saba zinakuwa 18,”amesema.
Katika sherehe hizo Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amezindua kitabu ambacho kinazungumza misingi ya muungano na maendeleo yake na kwamba kitabu hicho ni kitabu pekee tangu muungano ulipoanzishwa.
“Maelekezo yenu yamefanikisha hili, kitabu hichi kitakuwa ni nyenzo kwa Watanzania, nyenzo kwa wadau mbalimbali ya msingi, historia na maendeleo ya muungano katika miaka mbalimbali,” Waziri Jafo
Wakati huo huo Waziri Jafo amesema kama itampendeza kinaweza kutumika katika somo la historia shuleni ili kupandikiza agenda ya ufahamu kuhusu muungano wa Tanzania na Tanganyika.
No comments:
Post a Comment