Pages

Saturday, April 2, 2022

JUKWAA LA MITINDO KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

Mbunifu wa Mavazi nchini Ezra Emmanuel akizungumza na Waandishi Wahabari mara baada ya kutambulisha rasmi jukwaa la Mitindo linalotarajiwa kufanyika rasmi mara baada ya kumalizika Kwa mwezi mtukufu

Na.Khadija Seif, Michuzi TV

KATIKA kuendeleza na kuunga Mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan nchini, Mbunifu wa mavazi, Ezra Emmanuel anatarajia kuandaa jukwaa la Mitindo baada ya

kumalizika Kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Tamasha hilo la lenye lengo la kuwashika mkono wabunifu wanawake ambao wana ndoto za kufika kupitia mitindo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ezra Emmanuel ameeleza zaidi lengo la tamasha hilo ni kukuza vipaji vya vijana, pia kuendelea jitihada za Rais Samia katika kufikia Tanzania ya uchumi.

Aidha, Tamasha hilo litahusisha wabunifu wachanga na wakongwe kwa ajili ya kuonyesha mavazi yao.

"Tamasha hilo la mitindo litafanya badala ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kumalizika, pia nitakuwa na darasa la kutoa mafunzo ya ufundishaji wa nguo mbalimbali kwa vijana wenye ndoto za kuwa wabunifu."

Pia, mbunifu huyo amesema wabunifu watapaswa kumuunga mkono Rais Samia kwa kuwapa ajira vijana ili taifa liwe na idadi kubwa ya vijana ambao watafikisha nchi katika maendeleo kupitia vipaji vyao.

"Rai yangu kwa vijana kujitokeza kwa wingi katika darasa hili ili kuja kupata wakina Ezra wengine katika fani ya mitindo nchini".

Ezra ameweka bayana mafanikio yake  katika kipindi chote cha Miaka 15 amewabunia watu mbalimbali mashuhuli viongozi na kupata mialiko nje ya nchi ikiwemo Kenya kwa ajili ya kubuni mavazi.

No comments:

Post a Comment