Na Khadija Kalili
Chama Cha Waajiri nchini
(ATE) kimeahidi kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na wadau wake ambao ni Mashirika binafsi, watu wenye ulemavu pamoja na Serikali katika kusimamia masuala ya ajira .
Akizungumza leo katika Ofisi za ATE zilizopo Mikocheni Dar Es Salaam Meneja wa ATE Kanda ya Kati Dodoma Leonard Selestini alisema hayo katika mkutano uliowakutanisha na Jumuia ya watu wenye Ulemavu nchini ambao ni TASI,TLB na CHAVITA.
Wakizungunza kwa nyakati tofauti watu wenye ulemavu wamesema kuwa bado kunachangamoto nyingi katika utekelezwaji wa sheria ya kupata ajira.
Katibu wa Tanzania Albinism Society (TASI) Mussa Kabimba alisema kuwa "Tuko hapa kujadili sheria inayoihusu utekelezwaji wa upatikanaji wa ajira kwa watu wenye ulemavu nchini sababu bado kunachangamoto nyingi ambazo watu wenye ulemavu wanakumbana nazo katika upatikanaji wa ajira hivyo tuko hapa kujadili ili nao waweze kunufaika" alisema Kabimba.
Katika mkutano huo watu hao wenye ulemavu waliweza kutoa maoni mbalimbali na kuishauri ATE iweze kuweka utaratibu wa kufanya ufuatiliaji kwa watu wenye ulemavu pindi wanapoajiriwa hii itasaidia kung'amua changamoto wanazokumbana nazo.
No comments:
Post a Comment