Pages

Wednesday, March 30, 2022

Zaidi Ya Wastaafu 1000 Njombe,Wanufaika Na Mikopo Ya Benk Ya TCB

Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba akizungumza na watumishi wa benki ya TCB mara baada ya kutembelea banda la benk hiyo lililopo katika uwanja wa Sabasaba.

Meneja wa benki ya biashara tawi la Njombe Martin Wambali akieleza namna benk hiyo inavyofanya kazi kwa karibu na jamii huku akiwakaribisha wananchi kwa ajili ya huduma za benk hiyo.

Na Amiri Kilagalila,Njombe


Zaidi ya wastaafu 1000 mkoani Njombe wamenufaika na mikopo inayotolewa na benk ya biashara Tanzania (TCB) tawi la Njombe ili kuendelea kukamilisha ndoto za watumishi waliofikia ukomo wa umri wa utumishi wao.



Hayo yamebainishwa na meneja wa benki ya biashara tawi la Njombe Martin Wambali alipotembelewa na mkuu wa mkoa wa Njombe katika maonesho yanayoendelea uwanja wa Sabasaba mjini Njombe kuelekea uzinduzi wa mbio za mwenge kitaifa utakaofanyika katika uwanja huo hapo April 2 mwaka huu.

“Kwa mkoa wetu wa Njombe tunatoa sana mikopo ya wastaafu na benki yetu ni maarufu sana kwa kutoa mikopo ya wastaafu na zaidi ya wastaafu 1000 kwa mkoa wote wa Njombe”Alisema Wambali

Aidha ametoa wito kwa wastaafu kuendelea kuwa karibu na benki hiyo ili kutimiza ndoto zao kwa kuwa kustaafu sio mwisho wa kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba ameipongeza benk hiyo kwa ubunifu wa mikopo kwa wastaafu licha ya kutoa huduma zingine mbali mbali kwa jamii.

“TCB wamebuni kitu kizuri nafikiri ni jambo kubwa sana na wanafanya kazi nzuri hata hivyo kwa Njombe nimeona wamefungua tawi linguine hakika mnastahili pongezi”alisema Kindamba.
 

No comments:

Post a Comment