KAMPUNI ya vinywaji ya TBL inayomilikiwa na kampuni ya AB Inbev imeendelea na jitihada za kutafuta suluhu za changamoto mbalimbali za
Maendeleo kwenye jamii kwa kwa kutoa wito kwa wavumbuzi kujiunga na Programu yao ya Accelerator 100+Wito huo umetolewa leo Machi 31 2022 na Abigail Mutobiyerwa Meneja Masuala endelevu wa Kampuni ya TBL, kwa wavumbuzi kutoka mikoa yote nchini kujiunga na Program hiyo ili kutafuta suluhisho la changamoto kwenye jamii kwenye ugavi, utunzaji wa vyanzo vya maji na kilimo endelevu na mengineyo.
"Programu hii imedhamiria kuwezesha Kampuni ndogondogo zenye shauku ya kufanikiwa kwa kubuni na kuvumbua mawazo yenye tija kwenye jamii ili kutafuta suluhisho za changamoto za ugavi, utunzaji maji, kilimo, endelevu, mabadiliko ya tabia nchi, jkjaji wa pamoja na viumbe hai, amesema Abigail.
Amesema, katika miaka ya miwili iliyopita , programu hiyo imeziongezea uwezo kampuni 70 za kwenye nchi zaidi ya 20 na kuwajengea uwezo wajasiliamali wenye shauku kwa kuwasaidia kupeleka bidhaa zao sokoni kwa haraka.
Amesema kuwa rasmi TBL imefugua milango kwa kampuni chipukizi kwa ajili ya kujiunga kwa Program hiyo itakayowawezesha kupata mafunzo,Ushauri na pesa kiasi cha USD 100,000 kwa ajili ya kuendeleza miradi yao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Chanzi Ltd, Andrew Wallace ambaye aliwahi kuwa mshindi wa programu hiyo ameshiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao na kusema kupitia Accelerator 100+ wamekuwa wakikusanya chakula kinachotupwa na kukibadirisha kuwa chakula cha wanyama na mbolea halisi na kufanya kazi kubwa ya kuwezesha biashara nyingi kutafuta suluhisho za baadhi ya mambo ya kkmazungira yenye uharaka na changamoto za kijamii.
Aidha imeelezwa kwa waombaji wote watafanyiwa tathmini kwa awamu na salama zimetolewa ambapo mwisho kutuma maombi hayo ni tarehe 30 Aprili 2022 na kwamba maomb hayo yatumwe kupitia site ya www.100Accelerator.com
No comments:
Post a Comment