Mkuu wa wilaya ya Ilala Ng’wilaburu Ludigija (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa bima ya Hifadhi Biashara iliyoanzishwa na kampuni ya Howden Puri. Bima hiyo maalum kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Wamachinga.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) Dkt. Baghayo Abdallah Saqware akizungumza katika uzinduzi wa bima ya Hifadhi Biashara iliyoanzishwa na kampuni ya Howden Puri. Bima hiyo maalum kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Wamachinga.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bima a Howden Puri Sinda Sinda akizungumza katika uzinduzi wa bima ya Hifadhi Biashara iliyoanzishwa na kampuni ya Howden Puri. Bima hiyo maalum kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Wamachinga.
Mwenyekiti wa Chama Cha wafanyabiashara wadogo wadogo (Machinga) mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Namoto kizungumza katika uzinduzi wa bima ya Hifadhi Biashara iliyoanzishwa na kampuni ya Howden Puri. Bima hiyo maalum kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Wamachinga
Mratibu wa bidhaa wa kampuni ya Selcom, Gallus Runyeta akizungumza wakati wa uzinduzi wa bima ya Hifadhi Biashara iliyoanzishwa na kampuni ya Howden Puri. Bima hiyo maalum kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Wamachinga.
Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa Mshamma Mshamma akizungumza katika uzinduzi wa bima ya Hifadhi Biashara iliyoanzishwa na kampuni ya Howden Puri. Bima hiyo maalum kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Wamachinga.
Wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kwa jina la Wamachinga wakifuatilia uzinduzi wa bima ya Hifadhi Biashara iliyoanzishwa na kampuni ya Howden Puri.
Washirika wakuu wa Bima ya Hifadhi Biashara iliyozinduliwa na kampuni ya Howden Puri wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wialaya ya Ilala Ng’wilaburu Ludigija
Mkuu wa Wilaya akiwa na Washirika wa Bima ya Hifadhi BiasharaViongozi mbalimbali wa Hifadhi biashara
Kampuni ya Howden Puri imezindua bima maalum kwa wajasiriamali ijulikanayo kwa jina la Hifadhi Biashara, ambayo lengo kubwa ni
kulinda wafanyabiashara wadogo wanapopata majanga mbalimbali.
Kupitia Hifadhi Biashara, mfanyabiashara anaweza kuweka kuanzia sh 7,000 kwa mwezi kumwezesha kulinda mtaji wake endapo atapata majanga kama ya moto, wizi na mengineyo na kupata fidia hadi kiasi cha sh 5 milioni kuweza kuendelea na biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Howden Puri, Umesh Puri, Alisema kuwa wameamua kuweka bima yenye kiasi nafuu kabisa ili kuwawezesha wafanyabiashara wengi kujiunga na kuwa na matumaini ya kuendelea na biashara zao.
Alisema kuwa kwa kawaida gharama za bima ni ghali sana na kusababisha wafanyabiashara wadogo kushindwa kujilinda na majanga mbalimbali.
Alifafanua kuwa kampuni yao imeona tatizo hilo na kuja na utatuzi kwa wafanyabiashara hao kupitia maendeleo makubwa ya teknolojia na kulifanya suala la kujiunga na bima kuwa rahisi na kupatikana muda wote.
Mfanyabiashara haitaji kwenda ofisini kujiunga na huduma ya Hifadhi Biashara zaidi ya kutumia simu ya kiganjani kupitia TigoPesa USSD code *150*01#, app ya duka.direct na Selcom kupitia wakala yoyote nchini.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha wafanyabiashara wadogo wadogo (Machinga) mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Namoto alisema wafanyabiashara wengi walitetereka na wengine kufilisika kabisa wakati wa janga la Uviko-19 na moto katika masoko ya Kariakoo, Karume na Mwenge.
Bw Namoto alisema kuwa bima ya Hifadhi Biashara ni suluhisho la majanga yote kwa wafanyabiashara na kuwaomba kujiunga na kuwaomba kampuni ya bima kutoa huduma bora za madai wanapoletewa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa Mshamma Mshamma alisema kuwa wameamua kuingia katika huduma hii kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo kufanya huduma ya kulipa na kupokea malipo kupitia mtandao bora zaidi.
Naye, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Selcom Sameer Hirji alisema kuwa kampuni yao inajivunia kuingia katika huduma ya bima ya Hifadhi Biashara kutokana na kukuwa kwa sekta ya bima nchini na kuchangia uchumi.
Hirji alisema kuwa kampuni yao itatoa huduma bora yenye unafuu zaidi na kwani inatambua kuwa sekta ya bima mbali ya kuwalinda wafanyabiashara, pia inachangia kipato.
“Huduma hii lengo lake kubwa ni kusaidia maendeleo ya biashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo. Tunajisikia fahari kubwa kushiriki na kuwa mmoja wa wadau wa kuchangua maendeleo,”alisema Hirji. Mbali ya Howden Puri,Selcom, Tigo, wadau wengine katika huduma hiyo ni benki ya CRDB na kampuni ya bima ya Sanlam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilaburu Ludigija aliipongeza kampuni ya Howden Puri kwa ubunifu wenye tija kwa jamii na kuwaomba wafanya biashara wadogowadogo kujiunga na bima hiyo kwa faida yao.
Bw. Ludigija alisema kuwa dharura haina taarifa ya saa wala siku na kusisitiza wafanyabishara kujiunga na bima hiyo bila kusita.
“Kwanza naipongeza kampuni ya Howden Puri kwa ubunifu wenye lengo la kusaidia jamii ya wafanyabiashara wadogo wadogo. Hii ni fursa pekee kwa wafanyabiashara kwani bima hii itakuwezesha kuwa na uhakika zaidi ya kupata maendeleo hata kama utapata dharura mbalimbali na kusababisha kufirisika”alsema Ludigija.
No comments:
Post a Comment