Pages

Wednesday, March 30, 2022

AKUTWA NA HATIA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA MADINI BILA KUWA NA KIBALI.

Mnamo Machi 28, 2022 mtuhumiwa alipatikana na hatia kwa kosa la kupatikana na madini aina ya dhahabu bila kuwa na kibali na kutakiwa kulipa faini ya Tshs.1,000,000/= au miaka miwili jela. Pia imetolewa amri ya kutaifishwa kwa madini hayo pamoja na gari yenye

namba za usajili T.948 DTM aina ya Toyota Crown Anthlete yenye thamani ya Tshs.20,000,000/= hivyo kufanya jumla ya thamani ya mali yote iliyotaifishwa kuwa Tshs.189,745,766/=. Aidha kupitia Plea bargain agreement alilipa serikalini royalties, inspection fee pamoja na service levy kwa ujumla wake ya Tshs.11,548,407.24/=.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa COSTANTINE SOSPETER @ SAMBAJA [29] Mkazi wa Chokaa Halmashauri ya Chunya, mkoani Mbeya kwa kosa la kupatikana na madini aina ya dhahabu bila kuwa na kibali yenye uzito wa gramu 1,367.07 yenye thamani ya shilingi milioni 158,197,359.37 kinyume na kifungu namba 18 (1) na kifungu namba 4 (a) cha sheria ya madini namba 123 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 pamoja na kifungu namba 57 (1) na 60 (2) ya sheria ya uhujumu uchumi namba 200 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019. Pia kifungu namba 13 (1) (a) ya sheria ya utakatishaji fedha namba 423 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Awali mnamo Februari 9, 2022 majira ya saa 19:30 usiku huko katika kizuizi cha Polisi Chalangwa kilichopo Wilaya ya Chunya, Askari Polisi kwa kushirikiana na Maafisa madini wa Wilaya ya Chunya walimkamata COSTANTINE SOSPETER @ SAMBAJA [29] Mkazi wa Chokaa Halmashauri ya Chunya akitorosha Madini aina ya dhahabu yenye uzito wa gramu 1,367.08 yenye thamani ya shilingi milioni 158,197,359.37 akitumia gari aina Toyota Crown Anthlete.

No comments:

Post a Comment