WAKATI Mbio Maarufu za Kimataifa za Kilimanjaro zikiadhimisha Miaka 20 tangu kuasisiwa kwake, Watanzania wameonesha jeuri ya hali ya juu kwa kushinda nafasi nyingi sana za juu katika msimu huu ambapo Mtanzania Emmanuel Giniki ameibuka Mshindi wa Mbio za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon 2022 zilizofanyika mjini Moshi jana jumapili.
Giniki amevunja mwiko kwa mbio hizo na kuvunja na kuweka Rekodi ya Mtanzania mwingine Joseph Panga aliyeibuka Mshindi wa kawanza wa Mbio hizo mwaka 2020; ambazo kwa miaka kadhaa zimekuwa zikitawaliwa na raia wa kigeni na husasani Wakenya ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiibuka washindi.
Mshindi huyo nambari moja wa Mbio za Tigo Kili Half Marathon 2022 kwa upande wa wanaume ameshinda mbio kwa kishindo cha aina yake baada kuvunja Rekodi ya Mtangulizi wake Joseph Panga aliyeshinda kwa kumaliza Mbio hizo kwa kutumia 01:03:59 mwaka 2020, ambapo Giniki amemaliza Mbio hizo mwaka huu kwa kutumia muda mfupi zaidi wa saa 01:00:35 na hivyo kuleta hamasa kubwa sana mbele ya Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye mbio hizo!
Katika Mbizo hizo za Tigo Kili Half Marathon 2022, Giniki amefuatiwa na Watanzania wenzake Gabriel Geay na Inyasi Sulley waliotumia muda wa 01:02:05 na 01:04:11 na kuibuka washindi wa pili na wa tatu, huku wakufuatiwa na Kaposhi Laizer na Shing’Ade Giniki wote kutoka Tanzania walibuka washindi wa nafasi ya nne na tano.
Kufuatia matokeo hayo, Tanznaia imechukuwa nafasi za juu kuanzia ya kwanza hadi ya tano katika Mbio zaTigo Kili Half Marathon 2022 wakimwacha kwa mbali Mkenya Bernard Masau aliyeshika nafasi ya sita kwa kumaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa 01:04:56. Watanzania wameibuka washindi wa nafasi zote 8 kati ya kumu bora kwa upende wa Tigo Kili Half Marathon 2022 na kuwaacha kwa mbali wakenya waliobuka washindi wa nafasi ya sita na ya saba tu!
Akizungumza mara baada ya kumaliza Mbio hizo na kuibuka mshindi wa kishindo, Giniki anasema kuwa anayo furaha kushinda mbio hizo na kuiletea heshima nchi yake jambo ambalo amekuwa akilitamani, huku akiwashukuru waandaji na wafadhii za Mbio hizo za kiliometa 21 kwa miaka saba mfululizo sasa, Kampuni ya TIGO.
Giniki anaitaja siri ya ushindi wake nu mazoezi na kujituma, na kuendelea kufafanua anayo furaha kushinda mbio hizo na kuiletea heshima nchi yake jambo ambalo amekuwa akilitamani.
“Pamoja na kwamba mbio hizi zimekuwa zikifanyika hapa nyumbani, tumekuwa tukishindwa kuzitendea haki kwa kuwa wageni ndiyo wamekuwa wakizitawala. Ninayofuraha leo nimeweza kulitoa taifa langu kimasomaso,” alisema Giniki.
Katika mbio hizo za Kili Half Marathon mwaka huu, Watanzania wameng’ara sana ikilinganishwa na miaka ya nyuma, ambapo kwa wa wananwake, Mkenya Agness Ngolo ameibuka mshindi wa kwanza kwa kumaliza mbio hizo kwa kutumia muda 01:12:17 kwa kumpia kwa mbali kidogo Mtanzania alieyibuka Mshindi wa pili kwenye Mbio hizo, Jackline Sakilu alieyemaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 01:14:50.
Akizungumzia ushindi huo kwa upande wa wanawake mwanaraiadha Agness Ngolo kutoka Kenya alimeashukuru Waandaji wa mashindano hayo na wadahamini kampuni ya TIGO kwa kufanikisha masihndano hayo ambayo ni chachu kwake ya kushiriki mashindano mengine mbalimbali ndani nan je ya bara la Afrika.
Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi zawadi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Innocent Rwetabura anasema kampuni yake inayofuraha kuchangia maendeleo ya michezo nchini na hususani riadha ambayo pia huboresha afya.
Rwetabura anaendelea kufafanua kuwa, Kampuni ya TIGO imekuwa mdhamini wa mbio za Kili Half Marathon kwa kipindi cha miaka saba mfululizo na kuongeza kuwa itaendelea kudhamini pamoja na kuboresha mbio hizo kila mwaka.
“Napenda kuchukua fursa hii pia kuwapongeza wabunifu na waandaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon kwa kutimiza miaka 20. Ni ukweli usiopingika kuwa mbio hizi toka kuanziswa kwake zimetangaza vyema fursa za utalii Tanzania hasa Utalii katika kanda hii ya Kaskazini. Pia, mbio hizi zimekuwa na mchango mkubwa kwenye sekta ya michezo, hususani riadha,” analifafanua Rwetabura na kuongeza kuwa;
“Tumeshuhudia wanariadha wa Tanzania waliofanya vizuri kwenye kilometa 21 yaani Tigo Kili Half Marathon wakishinda na kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania kwenye mbio za Kimataifa. Tigo, tukiwa waadhamini wakuu wa Kilomita 21 (Tigo Kili Half Marathon) tangu mwaka 2015, tunajivunia kuwa sehemu ya mafanio tunayoyaona leo,”
Kaimu Mkurugenzi huyo aliendela kufafanua kuwa, sambamba na udhamini wa mbio hizi za Tigo Kili Half Marathon, mwaka jana walizindua mkakati wa utunzaji mazingira ujulikanao kama Tigo Green for Kili, One Step, One Tree wenye lengo la kuchangia uhifadhi wa mazingira yanayozunguka Mlima Kilimanjaro kwa kupanda miti 28,000.
“Hata hivyo, kutokana na mwitikio mkubwa wa wadau mbali mbali wa mazingira yakiwemo makampuni binafsi na mashirika ya serikali, tulipata michango na kununua miche ya miti zaidi ya 30,000 ambapo mwaka jana ikiwa ni awamu ya kwanza ya mradi tuliweza kupanda miche ya miti 11,000. Hivyo basi, mwaka huu ikiwa ni awamu ya pili ya mradi, tutapanda miche 20,000 ambapo jana kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Hai na wananchi wa eneo hili, tulizindua awamu hii kwa kupanda miche 1000 kwenye Kijiji cha Kwa Sadala. “ alifafanua Rwetabura.
Aliendelea kufafanua kuwa Kampuni ya TIGO imejizatiti kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora za mawaslinao zenye tija kwa jamii, kwa maendeleo ya taifa.
No comments:
Post a Comment