Pages

Thursday, February 3, 2022

Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi wa taasisi mbalimbali

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi. 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali. yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa Januari 27,2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said.

Mosi, kwa mujibu wa uteuzi huo ambao umeanza Januari 27, 2022, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Said Seif Mzee kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Rahma Salim Mahfoudh kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua, Akif Ali Khamis kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua CDR Mohamed Khamis Makame kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Meli Zanzibar katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

No comments:

Post a Comment