Pages

Thursday, February 3, 2022

MZUMBE DAR YATOA ELIMU JUU YA 'PERSONAL BRANDING'

Mtoa Mada, Carl bosser akizungumza na wanachuo wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo juu ya masuala ya Chapa binafsi (Personal Branding) kwa wadau wa Rasilimali watu na wanachuo wa masomo ya Rasilimali watu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akizungumza wakati wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding). yaliyotolewa kwa wanachuo wa Masomo ya Rasilimali watu chuoni hapo. kulia ni Mtoa Mada, Carl bosser na kushoto ni Mhadhiri chuo Kkinuu Mzumbe, Dkt. Seif MubaMratibu wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding), Dkt.faisal Issa akizungumza na wadau wa Rasilimali watu wanaosoma Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.

Mtoa Mada, Carl bosser akizungumza na baadhi ya wanachuo wa masomo ya Rasilimali watu wa Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding) yaliyofanyika jijini Dar es     Salaam.
Mmoja wa wanachuo akitoa ufafanuzi juu ya suala lililojitokeza wakati wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding).




Washiriki wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding) wakimsikiliza mtoa mada, Carl Bosser.

Msheheresaji wakati wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding) akitoa shukurani kwa Mtoa mada mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.

CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar  es Salaam yawajengea uwezo wanachuo wamasomo ya Rasilimali watu na wadau wa rasilimali watu kutoka taasisi mbalimbali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa mafunzo hayo mtoa Mada, Carl bosser amesema kuwa wasijisikie vibaya kujitathimini pale wanapojijenga kwajili ya kutambulika.

Amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo juu ya wananchuo na washiriki wengine juu ya kuwaimarisha juu ya  Chapa binafsi (Personal Branding) ya kile wanachokifanya.

Hata hivyo aliwaeleza umhimu watengeneza chapa binafsi zitakazo wafanya wajulikane zaidi kwa kile wanachokifanya kuliko  wanavyojijua wao wenyewe.

Bosser amesema kuwa chapa ni urithi wa maisha ambao kila mmoja anatakiwa kujiwekea katika ufanyaji kazi zake.

No comments:

Post a Comment