Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Donald Wright leo tarehe 2 February 2022 jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani katika sekta za afya, uwekezaji, biashara na uhusiano wa kimataifa.
|
No comments:
Post a Comment