Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James akisalimia na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakati wa Maadhimisho Siku ya Willness Day iliyoandaliwa na benki hiyo Kanda ya Mashariki kwa ajili ya wafanyakazi wake katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri Jamse akiongoza wafanyakazi wa Benki ya CRDB kupima afya wakati wa Maadhimisho Siku ya Willness Day iliyoandaliwa na benki hiyo Kanda ya Mashariki kwa ajili ya wafanyakazi wake katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Akizungumza katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri Jamse ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuja na program ya Willness ambayo itasaidia wafanyakazi kujua afya zao, kulinda afya zao na kuzijenga afya zao kupitia mazoezi jambo ambalo litaongeza tija katika kazi zao.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashari, Badru Idd, akipima urefu pamoja na uzito wakati wa maadhimisho ya Siku ya Willness Day iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Dar es Salaam (UDSM) jijini Dar es Salaan, mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Willness Day iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Dar es Salaam (UDSM) jijini Dar es Salaan, mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment