Baadhi ya wananchi waliofika Mliman City wakiendelea kuhudumiwa na BRELA ambao wamepiga kambi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi
Sehemu ya wananchi wakisubiri kuhudumiwa na maofisa wa BRELA waliopo Viwanja vya Mliman City ,Dar es Salaam
Mmoja wa maofisa wa BRELA akiendelea kumhudumia Mwananchi aliyefika kupata huduma.
Sehemu ya wananchi wakisubiri kuhudumiwa na maofisa wa BRELA waliopo Viwanja vya Mliman City ,Dar es Salaam
Mmoja wa maofisa wa BRELA akiendelea kumhudumia Mwananchi aliyefika kupata huduma.
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umeendelea kukutana na wananchi mbalimbali kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili ikiwa ni siku ya tatu tangu waweke kambi katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam kuwahudumia Watanzania.
Kwa mujibu wa Wakala huo kwa siku ya Januari 28, 2022 jumla ya Majina ya Biashara 26 na kampuni 7 yalisaliwa na baadhi yao kufanikiwa kupatiwa vyeti vyao pao kwa hapo.
Aidha baadhi ya wananchi ambao wamepata huduma zao na kutatuliwa changamoto zao wametoa pongezi kwa BRELA kwa namna walivyojipanga kutoa huduma huku wale walioaliofanikiwa kuondoka na vyeti vyao baada ya kusajili majina ya Kampuni na biashara wamesema waamehudumiwa kwa muda mfupi bila kuwatumia 'Vishoka'.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa cheti chake Armani Dior mbali ya kuonesha furaha aliyonayo kwa kupata cheti papo hapo ameiomba BRELA kuongeza elimu kwa wananchi kuhusu kutumia mifumo ya mtandao ili kuepukana na vishoka.
"Naiomba sana BRELA watusaidie kutoa elimu, hapa ukiangalia wengi walijaribu kusajili kwenye mtandao lakini kuna mahali walikwama, matokeo yake wale vishoka wanapata nafasi ya kufanya Biashara" amesema Dior na kuongeza ni vema utoaji huo huduma kama wanavyofanya Mliman City ukawa endelevu na wakaenda na mikoani.
Ametoa rai kwa wakazi wa Dar es Salaam kutumia fursa hiyo kupata elimu itakayosaidia kuepukana na vishoka wa mitaani. BRELA wapo kwenye viwanja ya Mlimani City kwa siku tano kuanzia Januari 26, na kufikia tamati Januari 30, 2022.
BRELA imeweka kambi eneo hilo kama mmoja ya mpango wake mkakati wa kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kufahamu umuhimu wa kusajili biashara majina ya biashara na Kampuni na kubwa wale wenye changamoto mbalimbali nazo kupatiwa ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment