Pages

Friday, December 31, 2021

Rais Samia Afanya Uteuzi Wa Viongozi Mbalimbali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali: -

1.     Amemteua Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita (06) kuanzia tarehe 17 Januari, 2022.

2.     Amemteua Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR). Balozi Mwinyi ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

3.     Amemteua Balozi Begium Kaim Taji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Arusha International Conference Centre (AICC). Balozi Taji ni Balozi Mstaafu wa Tanzania, Paris nchini Ufaransa

Teuzi hizi zimeanza tarehe 28 Desemba, 2021.


4.     Amemteua Bw. Patience Kilanga Ntwina kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Bw. Ntwina alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Katiba na ufuatiliaji wa Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.

 

Uteuzi huu umeanza tarehe 30 Desemba, 2021.

Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.


No comments:

Post a Comment