Pages

Wednesday, December 1, 2021

NAIBU KATIBU MKUU AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU, AWAASA KUENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu akizungumza kuhusu Serikali inavyothamini mchango wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu hivyo itasimamia taaluma hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ulioandaliwa na Bodi ya NBAA uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu alimwakilisha Waziri Wa Fedha na Mipango,  Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu akizungumza kuhusu namna alivyojipanga kama Mwenyekiti mpya pamoja na kusimamia ipasavyo Bodi hiyo ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ili kuendana na Kauli ya Rais Samia ya Kazi iendelee wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza kuhusu namna Bodi hiyo inavyofanya kazi pamoja na mafanikio waliyoyapata ndani ya muda mchache wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa, wanyakazi wa Bodi ya NBAA, Wahasibu na Wakaguzi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu aliyemwakilisha Waziri Wa Fedha na Mipango,  Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Wahasibu na Wakaguzi uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika Hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadhamini, Viongozi mbalimbali wa Serikali na Bodi hiyo pamoja na Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

No comments:

Post a Comment