Pages

Wednesday, September 29, 2021

KAMPUNI YA AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA

 
Mkurugenzi wa Airtel Money Isaac Nchunda (kushoto) Naibu Gavana katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dr. Bernard Y. Kibesse (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya I&M Baseer Mohammed (kulia) wakionyesha bango baada ya kuzindua huduma ya mkopo kwa kupitia simu za mkononi inayoitwa KAMILISHA ambapo wateja wa Airtel sasa wataweza kukamilisha miamala yao hata anapokuwa hana salio la kutosha kwenye akaunti yake ya Airtel Money.

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Money Isaac Nchunda akiongea leo jijini Dar es Salaam wakati wa huduma ya mkopo kwa kupitia simu za mkononi inayoitwa KAMILISHA ambapo wateja wa Airtel sasa wataweza kukamilisha miamala yao hata anapokuwa hana salio la kutosha kwenye akaunti yake ya Airtel Money.
   
*Yaingia ubia na benki ya I&M kuleta suluhisho la kifedha
   
    Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Airtel nchini kupitia huduma yake ya Airtel Money wameingia ubia na benki ya I & M Leo na kuzindua huduma ya mkopo kwa kupitia simu za Mkononi ambapo Wateja wa Airtel Sasa wataweza kukamilisha miamala yao.

Akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa kutangaza huduma hiyo , Naibu Gavana wa benki kuu nchini (BOT )Bernard Kibesse amesema siku zote benki kuu ipo kwa ajili ya kuwatia moyo taasisi au Makampuni yanayoingia ubia katika sekta za kibiashara ili kuongeza pato la taifa na kufikia uchumi wa kati na kuwaunga Mkono na kutoa mikopo ili kuleta suluhisho la kifedha kwa Watanzania.

"Natumaini ubia huu utaleta Manufaa kwa Makampuni haya mawili kwa kuona jinsi gani Wateja wao wanatumia huduma ya "Kamilisha" kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya Mahitaji yao kwa njia ya kidigitali yenye uharaka na wepesi kutumia.

Kibesse amesema benki kuu inawahimiza mabenki  Mengine na Mitandao ya simu kuiga mfano huo wa Kampuni ya Airtel Money pamoja na benki ya I &M wenye tija ambapo ameeleza benki kuu haitasita kutoa vibari kwa Makampuni yenye kuongeza pato la taifa kwa njia ya kifedha na kuwataka kushirikiana kwa ukaribu ili waweze kuwasaidia Wateja wao katika huduma za kifedha kwa njia ya kidigitali.

Aidha,Mkurugenzi wa Kampuni ya Airtel Money Isack Nchunda amesema "Dhamira ya Airtel Money toka awali imejikita zaidi katika kuleta huduma zenye suluhisho kwa Wateja wetu na ndio maana tumekuwa tukizindua huduma ambazo ni za ubunifu wa Hali ya juu kwa ajili ya kukidhi Mahitaji ya kila siku ya Wateja wetu hasa zile zinazohusu huduma za fedha kwavnjia ya mtandao."

Hata hivyo Nchunda ameeleza kwa namna gani huduma ya kamilisha itawanufaisha Wateja wa Airtel Money pamoja na benki ya I &M  kwa huduma za kifedha Pindi mteja anapoishiwa na Salio la kutosha kwenye akaunti yake ya Airtel Money.

"Kupitia utaratibu wetu wa kuwasikiliza Wateja,tumeweza kugundua kwamba Wateja wetu wanapata changamoto kwa sababu ya kukosa Salio la kutosha kwenye akaunti zao na hivyo kushindwa kufanya au kukamilisha baadhi ya miamala pale wanapohitaji kutuma fedha."

Pia ametaja huduma ambazo mteja wa Airtel Money ataweza kuzipata kupitia huduma ya "Kamilisha" pamoja na kulipia bili kama vile Luku,Dawasco na kutuma pesa kwenda Mitandao mingine,kununua muda wa maongezi .

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya I &M Baseer Mohammed ameongeza kuwa Ushirikiano huo na Kampuni ya Airtel ni moja ya mafanikio makubwa yenye ubunifu wa kidigitali,kwenye kutatua changamoto za kifedha kwa jamii kubwa yenye Sekta ya kibenki.

"Natumaini utakua Ushirikiano wenye kutatua changamoto za kifedha kwa Wateja wetu wa benki ya I&M  na hata Wateja wa Kampuni ya Airtel na itakua fursa kubwa kwenye huduma za kidigitali na inatoa uhakika wa kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa idadi kubwa ya Wateja"

No comments:

Post a Comment