Pages

Monday, August 30, 2021

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MAJENGO MAPYA YA JESHI LA POLISI MKOA WA SINGIDA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) akikata utepe kuzindua jengo jipya la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida leo. Wengine kutoka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Stella Rutabihirwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Siro, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Christopher Kadio.
 (Picha zote Dotto Mwaibale na Godwin Myovela)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua jengo jipya la ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.
Muonekano wa jengo hilo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua jengo la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Singida. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Siro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Stella Rutabihirwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Salamu ya Mkuu iliyoambatana na Wimbo wa Taifa kutoka 'Mounted Guard' ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Singida muda mfupi alipowasili Makao Makuu ya Kikosi hicho mkoani hapa kwa shughuli ya kuzindua moja ya jengo lake.






Muonekano ya jengo jipya la FFU Mkoa wa Singida.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Hayupo pichani) akipokea salamu kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Singida alipowasili kwa shughuli ya kuzindua moja ya jengo jipya la kikosi hicho.




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akikagua mradi wa jengo la FFU Singida muda mfupi kabla ya kulizindua.
Askari wa FFU wakiwa kwenye maandalizi ya kumpokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya kuwasili kuzindua jengo jipya la ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.
Afisa Mwandamizi kutoka Kampuni ya Biosustain mkoani Singida Abdulazizi Chaudhry na Wadau wengine mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wakuu wa Wilaya wakiwa kwenye uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagesa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida Diana Chilolo akiteta jambo na Mbunge wa Manyoni Mashariki Dkt.Pius Chaya.

No comments:

Post a Comment