Hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini Mswada wa Fedha wa 2021 inazidi
kuwakandamiza
wananchi ambao wanalazimika kugharimia ada mpya ya
asilimia 16. Aidha, wanawalaumu wabunge kwa kusalia kimya. Wanasema hali
hii imechangia talaka katika familia, wanawake wakikosa kabisa kuelewa
kuhusu kodi hiyo ya thamani.
Pia wameghadhabishwa na jinsi serikali inavyopandisha bei ya mafuta huku
ikishindwa kuchimba bidhaa hiyo katika eneo la Lokichar, Kaunti ya
Turkana. Mwanahabari wetu Mike Ekutan amefanya mahojiano na
wafanyabiashara, wahudumu wa bodaboda vilevile wasomi mjini Lodwar.
No comments:
Post a Comment