Pages

Saturday, July 31, 2021

ZANZIBAR YAPOKEA CHANJO YA COVID- 19 KUTOKA CHINA

Chanjo ya COVID-19  aina ya SINOVAC iliyopokelewa  katika Uwanja  wa Ndege wa Abeid A. Karume Zanzibar na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban kwa  niaba ya Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahamed Mazrui ikiwa ni msaada kutoka China

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban (kushoto) akipokea  Chanjo COVID-19 ya   aina ya SINOVAC kwa niaba ya Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahamed Mazrui  kutoka kwa Balozi Mdogo wa China Zhang Zhisheng (kulia)

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban akifafanua kuhusu chanjo ya COVID-19  aina ya SINOVAC  aliyoipokea kwa niaba ya Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee , Jinsia na Watoto Nassor Ahamed Mazrui  kutoka kwa Balozi Mdogo wa China Zhang Zhisheng (wa kwanza kulia) hafla iliyofanyika Uwanja wa ndege wa Abeid A. Karume Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Abdalla Sleiman Ali akijibu maswali ya Waandishi wa habari katika makabidhiano ya Chanjo ya aina COVID-19 ya SINOVAC kutoka kwa serikali ya china hafla iliyofanyika mara baada ya kuwasili Chanjo hiyo na ndege ya Ethopian katika Uwanja wa Ndege wa Abeid A. Karume Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA /MAEEZO ZANZIBAR.

 

No comments:

Post a Comment