Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza
wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Watoa Huduma wa
Simu Tanzania (TAMNOA), na kuwafafanulia kodi ya kizalendo ya miamala ya
simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania
kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini
Dodoma.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza wakati
wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba
(Mb) (hayumo pichani) na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania
(TAMNOA), walipofika wizarani hapo kwa, jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimsikiliza
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC Bw. Hisham Hendi, wakati wa
mazungumzo na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMOA), jijini
Dodoma.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC Bi. Rosalynn Mworia,
akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayumo pichani) na Chama cha Watoa Huduma
wa Simu Tanzania (TAMNOA) kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na
bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania
kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini
Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Mipango na Uwekezaji wa Vodacom Tanzania Plc
Bi. Hilder Bujiku.
Baadhi
ya wajumbe wa Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA)
wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck
Nchemba (Mb), (hayumo pichani), akizungumza wakati walipofika wizarani
hapo kwa mazungumzo kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando
za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia
mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Baadhi
ya wajumbe wa Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA)
wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck
Nchemba (Mb), (hayumo pichani), akizungumza wakati walipofika wizarani
hapo kwa mazungumzo kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando
za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia
mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Baadhi
ya Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mazungumzo kati
ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na
Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA) kuhusu kodi ya
kizalendo ya miamala ya simu na bando za mitandao inayotakiwa kuanza
kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya
maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Mkuu
wa Mipango na Uwekezaji wa Vodacom Tanzania Plc Bi. Hilder Bujiku
akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayumo pichani) na Chama cha Watoa Huduma
wa Simu Tanzania (TAMNOA) kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na
bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania
kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini
Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC Bi.
Rosalynn Mworia, baada ya mazungumzo na Chama cha Watoa Huduma wa Simu
Tanzania (TAMOA) kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na bando za
mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania kuchangia mapato
ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (wa nne
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Watoa Huduma
wa Simu Tanzania (TAMOA) kuhusu kodi ya kizalendo ya miamala ya simu na
bando za mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa kwa kila Mtanzania
kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi, jijini
Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
WAZIRI
wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb),
amekutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Watoa Huduma wa Simu
Tanzania (TAMNOA), na kuwaeleza kuwa kodi ya miamala ya simu na bando za
mitandao inayotakiwa kuanza kutozwa na mitandao ya simu ni ya kizalendo
inayolenga kila Mtanzania kuchangia mapato ya Serikali kwa ajili ya
maendeleo ya nchi.
Dkt.
Nchemba alisema kuwa Serikali imepanga kutekeleza miradi mingi ya
maendeleo ya wananchi na inayohitaji fedha nyingi na kwamba jukumu la
kukamilisha miradi hiyo ni la Watanzania wote wenye uchungu wa
maendeleo.
“Fedha
zitakazo patikana kwenye tozo hizo hazitatumika kulipa mishahara wala
kugharamia matumizi mengine yoyote ya Serikali bali zitapelekwa moja kwa
moja kutatua changamoto za afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara,
elimu na mingine mingi ikiwemo miradi ya kimkakati kama ujenzi wa reli
ya kisasa na Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere” alisema Dkt.
Nchemba.
Dkt.
Nchemba alisema kuwa jambo la kutia moyo ni kwamba Watanzania wengi
wameunga mkono kutozwa kodi hiyo kwa kutambua umuhimu wa maendeleo yao
ambayo kukamilika kwake kunahitaji mchango wao mkubwa.
“Kampuni
za simu msichukulie makato haya kama kodi nyingine mnazowatoza wateja
wenu bali Serikali iliamua kuweka makato haya kwenye miamala ya kuweka
muda wa maongezi na kufanya miamala kwa njia ya simu ili kuwafanya
Watanzania na watumiaji wengine wa simu kuchangia maendeleo ya
nchi”alisisitiza Dkt. Nchemba.
Dkt.
Nchemba alitoa muda wa siku 14 kuanzia tarehe 1 hadi 15 Julai, 2021,
kwa watoa huduma wote wa Mitandao ya Simu kurekebisha mifumo yao na
kuanza kutoza rasmi makato hayo ili Serikali ianze kukusanya fedha hizo
ambazo amesema zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuwakwamua
wananchi kutoka katika adha mbalimbali.
Kwa
upande wao Chama cha Watoa huduma za mitandao ya simu, waliiomba
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iwape muda wa kurekebisha
mifumo yao itakayotumika kukusanya tozo hizo kwa kuwa zoezi hilo
linahitaji muda wa kiufundi.
Akizungumza
kwa niaba ya Chama hicho, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya
Vodacom Bi. Roselynn Mworia, alisema kuwa chama chao kimeupokea mpango
huo kwa mikono miwili na kuwataka wateja wao kuiunga mkono Serikali kwa
kuendelea kutumia huduma za kupiga simu na kufanya miamala ya simu.
“Lengo
la Serikali la kuamua kukusanya fedha za maendeleo kwa njia hiyo ni
zuri kwani litaharakisha utekelezaji wa miradi ya huduma za kijamii, kwa
kweli ni kodi ya kizalendo” alisema Bi. Mworia.
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi karibuni, lilipitisha tozo ya
kuanzia shilingi 10 hadi shilingi 10,000 kutozwa katika kila muamala wa
kutuma au kupokea pesa na kiwango cha shilingi 10 hadi 200 kwa siku kila
mteja anapoongeza salio la muda wa maongezi kwenye simu ambapo kwa
pamoja, Serikali inatarajia kukusanya wastani wa shilingi trilioni1.7
kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment