Moja
ya eneo la mradi wa umeme wa maji ya mto Ruhudji sehemu ambayo
itajengwa bwawa kubwa likionekana kwa umbali wakati bodi ya wakurugenzi
ilipofika na kujionea eneo la mradi huo.
Dkt.Alexander
Kyaluzi mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TANESCO akitoa maagizo kwa
wataalamu wa mradi ili kuongeza kasi ya ujenzi huku akieleza pia faida
za bodi hiyo kutembelea katika eneo la mradi.
Bodi
ya wakurugenzi wa TANESCO wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa
wa Njombe Marwa Rubirya walipofika mkoani Njombe kwa lengo la
kutembelea miradi ya umeme inayojengwa mkoni humo.
Na Amiri Kilagalila,Njombe
Agizo
hilo limetolewa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TANESCO
Dkt.Alexander Kyaluzi wakati bodi hiyo ilipotembelea na kuona mahali
utakapojengwa mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 358.
"Wataalamu
wa mradi huu waende kasi zaidi kwasababu huu mradi unategemewa sana na
viongozi wetu wameshauzungumza mara nyingi kwa hiyo tungependa
utekelezwe kwa muda mfupi iwezekanvyo,kwa hiyo tungeomba wataalamu wetu
kila hatua waifikie kwa haraka zaidi"alisema Dkt.Alexander Kyaluzi
Aidha
Dkt.Kyaluzi amesema lengo la bodi hiyo kutembelea katika mradi muhimu
na tegemeo kwa tofauti ni pamoja na kuutambua zaidi ili kuelewa namna
unavyotekelezwa pamoja na bajeti zake.
"Lengo
letu ilikuwa ni kuja kuona changamoto zake za kufika hapa site
kwasababu wakati mwingine bodi mtaletewa taarifa ya kupitisha fedha
halafu mnasema hizi hela ni nyingi sana.Kwa hiyo ziara imetusaidia
kupata taarifa ili wakati tunapitisha makadirio basi tunakuwa na kumbu
kumbu"alisema Dkt,Kyaluzi
Kwa
upande wake mhandisi Toto Zedekia msimamizi wa muda wa mradi huo licha
ya kupokea maelekezo ya bodi ya wakurugenzi wa TANESCO,amesema mradi huo
muhimu unaotarajiwa kujengwa kwa miezi 36 utakuwa ni miongoni mwa
miradi muhimu nchini kwa kuwa maji ya mto huo hayakauki mwaka mzima.
"Mwaka
1998 ndipo ulipofanyika upembuzi yakinifu kwa hiyo kutokana na study ya
mradi huu tumejihakikishia kwamba kuna maji ya kutosha kwasababu
tunapima maji kila wakati na tumejiridhisha yapo wakati wote wa
mwaka"alisema Toto Zedekia
Vile
vile amesema licha ya kuchelewa kwa mradi huo lakini wanatarajia
kufanya kazi kwa kasi na kwa sasa wamekuwa wakisubiri bajeti ili mradi
huo uweze kuanza.
Baadhi
ya wananchi wanaozunguka mradi huo akiwemo Ibrahim Kilasi wamesema wapo
tayari kuendelea kutunza mto huo na mito mingine midogo inayoingiza
maji katika mto ruhudji ili kuwezesha umeme utakaozalishwa katika mradi
huo kuwa wa kudumu kwa kuwa utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa
Njombe na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment