Mkurugenzi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania (TKLNT), Isaac Mpatwa akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma leo.
Charles James, Michuzi TV
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa nne wa maombi ya kitaifa
utakaofanyika
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania (TKLNT), Isaac Mpatwa ambao ndio waanzilishi na waandaji wa mkutano huo kwa hapa nchini ambao utaanza kuanzia saa moja hadi saa tano za asubuhi kwa tarehe iliyopangwa.
Akizungumzia mkutano huo leo mbele ya wandishi wa habari, Mpatwa amesema kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni, "Utawala Bora na Uadilifi katika Uongozi" ambapo amesema kauli hiyo inaendana na mtazamo wa Serikali ya Rais Samia ambaye amekua akisisitiza utawala bora, uwajibikaji na ufuataji wa sheria kwa viongozi na wananchi.
" Serikali yetu inafahamu kuwa misingi hii ndio nguzo muhimu ya maendeleo ambapo mkakati wa kitaifa wa maendeleo wa mwaka 2021/25 umeweka wazi kuwa utawala bora na kufuata sheria ni mojawapo ya misingi muhimu ya maendeleo ya kiuchumi," Amesema Mpatwa.
Amesema mkutano huu ni wanne tokea kuanzishwa kwake mwaka 2016 na utahudhuriwa na viongozi kutoka Nchi mbalimbali wapatao 500 ukiwahusisha viongozi wa kiserikali, taasisi za dini, mashirika ya umma na binafsi pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.
" Msemaji Mkuu katika mkutano huu anatarajiwa kuwa Dk Bill Winston ambaye ni mwandishi wa Marekani ambapo pamoja na kufanya maombi kwa Nchi yetu na kujadili kuhusu utawala bora pia tutazindua kituo cha kulea wafanyabiashara wadogo na pia jukwaa Maalum la Wafanyabiashara kutoka Tanzania na Marekani kukutana na kubadilishana uzoefu." Amesema Mpatwa.
No comments:
Post a Comment