Mgeni
Rasmi wa Mkutano Mkuu wa Uchumi na Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke
Mwenye Ulemavu Tanzania, Dk Tulia Ackson akizungumza wakati wa mkutano
huo uliofanyika jijini Dodoma, jana. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju na Mwenyekiti wa Taasisi iliyoandaa
mkutano huo ya Ikupa Trust Fund, Stella Ikupa (wa tatu kushoto)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya ABC, Imani John Bgoya akizungumza wakati wa
Mkutano Mkuu wa Uchumi na Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu
Tanzania uliofanyika jijini Dodoma, jana. Katikati ni Mgeni Rasmi wa
mkutano huo, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson. Mkutano huo
uliandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Ikupa Trust Fund.
Baadhi
ya watendaji wa Benki ya ABC wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi na Mapendekezo ya Siku
ya Mwanamke Mwenye Ulemavu Tanzania uliofanyika jijini Dodoma, jana.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula
akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya ABC,
Imani John Bgoya pamoja na Watendaji wa benki hiyo mara baada ya Mkutano
Mkuu wa Uchumi na Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu
Tanzania uliofanyika jijini Dodoma, jana.
====== ======= ======
HOTUBA
YA MKURUGENZI MTENDAJI BANCABC KWENYE KONGAMANO LA SIKU MOJA JIJINI
DODOMA KUHUSIANA NA KUCHOCHEA UCHUMI TEGEMEZI KWA WATU WENYE ULEMAVU
TAREHE 28 JUNI 2021
Ndugu Mgeni Rasmi Mh Deputy Speaker (Naibu Speaker) Dr. Tulia Ackson,
Wabunge walikwa
Mwenyekiti wa Ikupa Trust Fund,
………………………………………………
Wateja wa BancAbc,
watu wenye ulemavu,
Waandishi wa Habari,
Wafanyakazi wenzangu,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana,
Habari za Asubuhi/Habari za Mchana,
Ni
heshima kubwa kwangu kusimama mbele yenu kwenye kongamano hili ambalo
nia yake ni kuwajengea uchumi tegemezi kwa watu wenye ulemavu. Sisi
BancABC tunayo furaha kubwa kuungana na Ikupa Trust Fund kuwawezesha
watu wenye ulemavu kupata haki ya elimu, maarifa pamoja na ujuzi kwa
kuwajengea uwezo wa kufikia mafanikio yao na familia zao ili wamudu
kujikimu kimaisha wakati wowote.
Uamuzi
wa serikali kurekebisha sheria ya fedha ya LGA ya kutenga asilimia kumi
kwa ajili ya Wanawake na vijana na sasa kuwajumuisha watu wenye ulemavu
ni moja ya sababu kubwa inayodhihirisha kwamba kundi linapaswa kupewa
kipaumbele sio tu na serikali bali pia na jamii kwa ujumla na ndio
sababu sisi BancABC, pia tumeunganisha nguvu na Ikupa Trust Fund ili
kuweza kufanikisha kongamano hili la siku mbili ili mafanikio yake
yaweze kuleta suluhisho la kifedha kwa watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa
Mgeni Rasmi, BancABC kwa kushirikiana na serikali imejizatiti
kuendeleza suluhisho la kifedha kwa kutanua wigo wa huduma za kifedha na
kuzileta karibu na wananchi wa Tanzania kwa nia ya kupunguza idadi ya
wananchi ambao hawajafikiwa na huduma za kifedha na kusaidia kuinua
maisha ya wananchi kwa kuongeza upatikanaji wa huduma zetu hapa nchini
Tanzania. Mwaka 2018, BancABC ilizindua tawi lake hapa Dodoma kwa lengo
hilo hilo, Pia hadi leo tunavyoongea hapa, BancABC tunazo ofisi 10 ndogo
za mauzo ambazo zinatoa huduma ya mikopo kwa wafanyakazi wa serikali
kwa mkoa huu wa Dodoma.
BancABC
iko kwenye mazungumzo na wadau ili kuja na pendekezo la dhamana kwa
huduma za kifedha kwa watu wenye ulemavu hapa nchini.
Tukiwa
na lengo la kuongeza chachu kwa watanzania kujua na kuwa na utamaduni
wa kuweka akiba, kupata riba na kisha kukopa, tumeweza kuzindua huduma
ambazo zinawafanya wateja wetu kupata riba kutoka kianzio cha chini cha
10,000 na kisha baadae kukopa kulingana na amana yake na hivyo kuweza
kuwawezesha wateja wetu kifedha.
BancABC
tunaedelea kuongeza suluhisho katika sekta ya huduma za kifedha kupitia
huduma zetu mbalimbali tunazotoa kwa wateja wetu nchini wa soko la
kawaida na hata wale wa makampuni tanzu kupitia kwenye matawi yetu yote,
mawakala wetu zaidi ya 300 pamoja na ofisi zetu ndogo za mauzo zaidi ya
100 zilizoenea kote nchini. Kwa kupitia njia hii tumefanikiwa kusambaza
huduma, na kuwafikia Watanzania walio wengi. Kupitia BancABC Mobi USSD
na applikesheni, huduma za benki kwa njia ya mtandao ambazo
zinawawezesha wateja wetu kupata huduma za kutoa fedha, kuweka na kupata
riba wakiwa popote pale.
Vile
vile tunazo kadi za malipo ya kabla ambazo zinapatikana kwenye sarafu 6
ambazo zinawawezesha wateja kufanya malipo bure kwa njia ya mtandao na
kwenye vituo vya malipo yaani POS. Vile vile wanaweza kutoa fedha kwenye
mashine za ATM za VISA wakati wowote na popote duniani.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
Nikudhihirishie
kwamba kwa hayo yote BancABC imedhamiria kuendelea kuunga mkono watu
wanaoishi na ulemavu kwa sababu afya na ulemavu ni moja ya lengo letu
Kubwa la kuweza kurundisha kwa jamii.
Mwaka
2018 tulishirikiana na Ikupa Trust Fund kuadhimisha Siku ya Wanawake
Duniani – kupitia tukio hilo la kila mwaka lenye lengo la kuongeza
uelewa kwa watu wenye ulemavu – kukuza maendeleo yenye ujumuishi na watu
wenye ulemavu kwenye jamii. Sisi bado tutaendelea kuja na ubunifu zaidi
wa mbinu tofauti tofauti ili kukuza ushirikiano huu zaidi na kufanya
kazi sambamba na malengo ya serikali kwa lengo la kuendelea kuleta
suluhisho la huduma za kifedha kwa makundi yote hapa nchini.
Asanteni sana kwa kunisikiliza na tunaungana na kauli mbiu ya sasa ‘Kazi iendelee’
No comments:
Post a Comment