Afisa
Sheria kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa wanawake, Rodger Michael
akizungumza leo na wananchi wa kata ya Tandika mtaa wa Nyambwera
walipofika WLAC kutoa elimu ikiwa ni njia mojawapo ya kusheherekea siku
ya wafanyakazi duniani ambayo hufanyika kila mwaka.
Mwananchi wa Mtaa wa Nyambwera akizungumza katika uhamasishaji wa kuijua sheria na haki kwa wafanyakazi wa sekta rasmi na sekta zisizo rasmi ngazi ya jamii akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nyambwera leo Mkoani Dar es Salaam.
Kushoto ni mmoja ya wahamasishaji wa kuijua sheria na haki kwa wafanyakazi wa sekta rasmi na sekta zisizo rasmi ngazi ya jamii akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nyambwera leo Mkoani Dar es Salaam.
Mwananchi wa Mtaa wa Nyambwera akizungumza katika uhamasishaji wa kuijua sheria na haki kwa wafanyakazi wa sekta rasmi na sekta zisizo rasmi ngazi ya jamii akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nyambwera leo Mkoani Dar es Salaam.
Kushoto ni mmoja ya wahamasishaji wa kuijua sheria na haki kwa wafanyakazi wa sekta rasmi na sekta zisizo rasmi ngazi ya jamii akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nyambwera leo Mkoani Dar es Salaam.
Moja
ya wahamasishaji wa kuijua sheria na haki kwa wafanyakazi wa sekta
rasmi na sekta zisizo rasmi ngazi ya jamii akizungumza na wananchi wa
mtaa wa Nyambwera leo Mkoani Dar es Salaam.
WAFANYAKAZI wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC)
washeherekea siku ya wafanyakazi kwa kutoa elimu kwa wananchi wa kata ya Tandika Mtaa wa Nyambwera Mkoa wa Dar es Salaam.Akizungumza
wakati wa kutoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa Nyambwera, Afisa Sheria
kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC), Barcoal
Deogratius leo Mei Mosi, 2021 amesema kuwa lengo la kutoa Elimu kwa
wananchi hao ni kutaka sheria ya ajira iweze kuenea kila mahali ili kila
mwananchi aweze kujua wajibu wao.
"Siku
ya leo tunaadhimisha simu ya wafanyakazi duniani WLAC tumekuja kata hii
ya Tandika mtaa wa Nyambwera kutoa elimu ya sheria ya mahala pa kazi
kwa wafanyakazi wa ndani pamoja na wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi na
sekta rasmi." Amesema Deogratius
Amesema
kuwa katika kumalizia muda wa miaka miwili wa Mradi wa uwezeshaji wa
jamii kisheria juu ya sheria na haki mahala pa kazi unaofadhiliwa na
shirika la Legal Services Facility wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi
mitaani kupitia ofisi za Serikali za mtaa yao.
"Leo
kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wananchi licha ya kuwa na hali ya hewa
ya Mvua katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam wananchi
wamekuja kutusikiliza na kujua ni nini tunawafundisha juu ya Masuala ya
Sheria na haki mahala pa kazi." Amesema Deogratius
Hata
hivyo Deogratius amesema wananchi wanatakiwa kujua haki zao mahala pa
kazi haijarishi upo katika sekta rasmi ama sekta isiyo rasmi.
Kwa
upande wake mwananchi wa Mtaa wa Nyambwera, Mwanaid Salum amesema kuwa
ametambua baadhi ya sheria ya ajira na atachukua kama faida kwake na
kuwafundisha watu wengine wanaowanyanyasa wafanyakazi.
Nae
Mkazi wa Mtaa wa Nyambwera, Idd Ramadhan ameowaomba wafanyakazi wa
Kituo cha Msaada wa Kisheria (WLAC) kuandaa mafunzo mengine ili wananchi
waweze kuelewa zaidi haki zao.
Wafanyakazi
wote wa sekta rasmi na sekta zisizo rasmi wanahaki sawa kwani sheria
mama ni moja tuu inayoongoza katika masuala mazima ya haki na usawa
mahala pa kazi nayo lazima ifuatwe." Amesema Deogratius
Licha
ya hayo katika kipindi cha Maswali na majibu wananchi wameweza kuuliza
maswali ya sheria ya ardhi, sheria za ndoa pamoja na sheria za Mirathi
kwa wanafamilia.
No comments:
Post a Comment