Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akiwaasa wamiliki wa Kampuni za Biashara nchini kutumia fursa hiyo kuutangaza Utalii wakati wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yanayofanyika leo jijini Mwanza.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Nchemba akipokea vitabu kutoka kampuni ya Global Education Link kabla ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yaliyofanyika leo jijini Mwanza. pembeni yake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Massanja akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa serikaliWaziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja kabla ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yanayofanyika Jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja ametoa wito
kwa Wafanyabiashara na wamiliki wa Makampuni mbalimbali hapa nchini
kuunga mkono juhudi za Serikali za kutangaza Utalii na vivutio
mbalimbali vilivyopo hapa nchini kupitia biashara zao.
Mhe.
Mary Masanja ametoa wito huo leo Jijini Mwanza, wakati wa maonesho
ya Biashara ,Uwekezaji na Utalii yanayowahusisha wadau mbalimbali.
Amesema wafanyabiasha ni wadau wakubwa wa utalii hivyo wana nafasi kubwa
ya kuutangaza utalii hatua itakayosaidia kuongeza idadi ya Watalii.
"Nawaomba
sana ninyi wafanyabiashara, kupitia makampuni yenu mtangaze Utalii wa
Tanzania na vivutio vyake ,ninyi ni wadau wakubwa wa utalii "amesema
Mhe. Mary Masanja.
Amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa wanapaswa
kutambua kuwa Sera ya Tanzania ya Viwanda itaendelea kutekelezwa kama
ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amekua akiwasisitiza Watanzania wawekeze katika miradi mbalimbali ya
maendeleo "
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Mashimba Ndaki ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo
amesema wafanyabiashara wakishirikiana vizuri wataweza kukuza uchumi wa
nchi pia kuutangaza utalii.
Aidha, amesema Serikali inaendelea
kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali ikiwemo uondoaji wa urasimu na
ukiritimba kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza hapa nchini.
"Serikali
tunaendelea kuziondoa changamoto kuziondoa changamoto zote
zinazolalamikiwa na wafanyabiasha na wawekezaji,tuvute subira kidogo
haya mambo yatakwenda kurekebishwa vizuri "amesema Mhe. Mashimba
Hatahivyo,
amezitaka Mamlaka za Serikali za mitaa kutengeneza wafanyabiashara
watakaolipa mapato kwa kuwapatia maeneo watakayo fanyia Biashara Ili
waweze kulipa kodi na kukuza uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment