Pages

Friday, April 30, 2021

ZOEZI LA UPANDISHAJI WA VYEO NA UBADILISHAJI WA KADA WATUMISHI WA UMMA (RECATEGORIZATION) KWA MWAKA 2020/21

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA


YAH: ZOEZI LA UPANDISHAJI WA VYEO NA UBADILISHAJI WA KADA WATUMISHI

(RECATEGORIZATION) KWA MWAKA 2020/21

Unapojibu tafadhali taja 

Kumb: Na BC.4697/03"D"/59

Makatibu Wakuu,

Makatibu Tawala wa Mikoa,

Wakuu wa Idara za Serikali Zinazojitegemea,

Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali,

Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Miji,

Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya,

Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma.

YAH: ZOEZI LA UPANDISHAJI WA VYEO NA UBADILISHAJI WA KADA WATUMISHI

(RECATEGORIZATION) KWA MWAKA 2020/21

Tafadhali husikeni na somo lililotajwa hapa juu.

2.         Ninapenda kuwataarifu kuwa idhini ya kupandisha vyeo watumishi waliotengewa katika Ikama na Bajeti kwa Miaka ya Fedha Miaka ya Fedha 2018/2019, 2019/2020 na 2020/2021 pamoja katika Ikama na Bajeti ya Mwaka 2020/2021 imetolewa kwa...

waajiri na kuwabadilisha kada (Recategorization) watumishi waliotengewa

3.         Kwa madhumuni ya ya kuhakikisha zoezi la upandishaji vyeo linafanyika kwa ufanisi na kwa wakati, mnaelekezwa kuzingatia sifa na vigezo vyote vilivyoainishwa katika Miundo ya Utumishi ya kila Kada pamoja na mambo yote yaliyoainishwa katika Kanuni D.51 (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, Toleo la Mwaka 2009 ikiwa ni pamoja na Tange (Seniority List) iliyohuishwa, kuwepo kwa nafasi iliyoidhinishwa katika Ikama na utendaji mzuri wa kazi kwa mujibu wa matokeo ya Tathmini ya Utendajı Kaz: (OPRAS).

Pamoja na sifa na vigezo hivi, watumishi wanaotakiwa kupandıshwa vyeo ni wa makundı

yafuatayo:-

(i)     Watumishi waliokasimiwa katika Ikama na Bajeti kwa Miaka ya Fedha 2018/2019, 2019/2020 na 2020/2021.

(ii)      Watumishi wa ajira ya mara ya kwanza ambao wameshathibitishwa kazini kwa mujibu wa Kanuni D.40 (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Mwaka 2009 na wametumikia vyeo vyao kwa muda usiopungua miaka minne (4) baada ya kuthibitishwa kazini;

(iii)    Watumishi wengine ambao wametumikia vyeo walivyonavyo kwa muda usiopungua miaka minne (4);

(iv)   Watumishi wenye utendaji mzuri wa kazi kwa mujibu wa matokeo ya Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) wenye alama zisizopungua tatu (3) au alama zinazofanana hizo kwa taasisi zinazotumia mifumo mingine ya kutathm ni utendaji kazı wa watumishi; na

(v)        Watumishi waliohakikiwa vyeti vyao na kuthibitika kuwa ni halali.

4.         Kuhusu zoezi la ubadilishaji kada watumishi (Recategorization) kwa nafasi zilizoidhinishwa kwenye bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/2021, mnasisitizwa kuzingatia matakwa ya Waraka wangu wenye Kumb. Na. C/AC.44/45/01/A/83 wa tarehe 01 Desemba. 2009 kuhusu utaratibu wa Kuwabadilisha Kazi (Recategorization) watunıshi wa ojiendeleza kielimu kama ilivyoainishwa katika Miundo ya kada zao pamoja na masharti yalıyoelekezwa katika Kanuni D.6 (2) ya Kanunı za Kudumu katika Utumishi wa Umma, Toleo la Mwaka 2009. Aidha, zoezi ia kuwabadilisha kada (Recategorization) linawahusu watumishi waliokasimiwa katika Ikama na Bajeti ya mwaka 2020/21 na si vinginevyo.

5.         Hata hivyo, mnaelekezwa kuwa zoezi la kuwapandisha watumishi vyeo na kuwabadilisha kada watumishi (Recategorization) halitawahusu watumishi wa makundi yafuatayo:-

(i)         Watumishi wenye vyeti vya elimu ya Kıdato cha Nne vinavyotambuliwa na Taasisı ya Elimu ya Watu Wazima walioajiriwa kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 lakıni hawajafanya na kufaulu mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne unaosimamiwa na NECTA kama nilivyoelekeza katika Aya ya CFB.228/290/01/"Y"/144 ya tarehe 24 Septemba, 2018; 5 (c) ya barua yangu yenye Kumb.

(ii)        Walimu wenye Astashahada ya Ualimu (Daraja la IIIB na IC) walioajirwa kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 ambao hadi sasa hawajajiendeleza katika kada ya Astashahada ya Ualimu (Daraja IIIA) au kupitia Mpango wa Mafunzo ya Ualımu Kazını (MUKA) kama nilivyoelekeza kwenye Aya ya 5(f) ya barua yangu yenye Kumb. Na. CFB.228/290/01/"Y"/144 ya tarehe 24 Septemba, 2018;

(iii)       Walimu wenye Astashahada ya Ualimu (Daraja A) walioajiriwa kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 ambao hawana elimu ya Kidato cha Nne au kupitia mpango wa Mafunzo ya Ualimu Kazini (MUKA) kama nilivyoelekeza kwenye Aya ya 5(g) ya barua yangu

yenye Kumb. Na. CFB.228/290/01/"Y"/144 ya tarehe 24 Septemba 2018,

(iv)       Watumishi wenye Mashauri ya kinidhamu, walioko masomoni kwa muda mrefu (Full Time), walioko Likizo bila Malipo na watumishi wenye ajira za mikataba (Employment on Contracts); na

(v)        Watumishi wa kada za Mtendaji wa Kata na Afisa Tarafa ambao utaratibu wao wa kubadilishwa kada (Recategorization) ulielekezwa katika Waraka wangu wenye Kumb Na. CCA.271/431/01/"H"/67 wa tarehe 01 Agosti, 2019 Aya ya 3(a). (b) na (c)

6. Makatibu Wakuu mnakumbushwa kusimamia ipasavyo zoezi hili kwenye Taasisi zilizo chini ya Wizara zao hususan zile ambazo hazitumii Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS). Aidha, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wasimamie zoezi la upandishaji vyeo na ubadilishaji kada kwa watumishi wenye sifa na vigezo stahiki wa Hospitali Teule za Wilaya (CDH) na Mashirika ya Dini ya Kujitolea (VAH) zilizopo katıka Halmashauri zao.

7. Kwa lengo la kuepuka kuzalisha madeni ya mishahara isivyostahili, waajiri mnaelekezwa kuhakikisha kuwa barua za upandishaji vyeo/ubadilishaji kada zikamilishwe na kuingizwa kwenye Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kabla ya tarehe 12 Juni, 2021. Hivyo, Kamati/Bodi za Ajira za kila Taasisi zinatakiwa zikamilishe uidhinishaji wa watumishi wanaopandishwa vyeo na kubadilishwa kada kabla au ifikapo tarehe 31 Mei, 2021.

 

Ninawashukuru kwa ushirikiano wenu.

Dkt. Laurean J. P. Ndumbaro

KATIBU MKUU (UTUMISHI)

Nakala kwa: Katibu Mkuu Kiongozi,

Ofisi ya Rais,

IKULU,

1Barabara ya Julius Nyerere,Chamwino,

S. L. P. 1102,

40400 DODOMA.

Nakala kwa:

Katibu Mkuu,

Wizara ya Fedha na Mipango.

Jengo la "Treasury Square",

S. L. P. 2802, 40468

DODOMA.

 

No comments:

Post a Comment