Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Na. 8 ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Na. 8 inayoshughulika na masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala akiongoza Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala Afrika kwa njia ya mtandao.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati Na. 8 ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Na. 8 inayoshughulika na masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa na Wajumbe wa Mkutano wa Wataalamu kutoka katika Ofisi yake, Bi Agnes kisaka Meena Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera (Wa kwanza kushoto kwake) na Bi Ellen Maduhu, Mkurugenzi Msaidizi wa Uchambuzi Sera wakati akiongoza Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala kwa njia ya mtandao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Na. 8 ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Na. 8 inayoshughulika na masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala akiwa na Wajumbe wa Mkutano wa Wataalamu kutoka katika Ofisi yake, Bi Agnes Kisaka Meena (Wa kwanza kushoto kwake) na Bi Ellen Maduhu, mara baada ya Mhe. Mchengerwa kuhitimisha Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala uliofanyika kwa njia ya mtandao.
…………………………………………………………………..
Na. Mary Mwakapenda-Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Na.8 ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Na. 8 inayoshughulika na masuala
ya Utumishi wa Umma na Utawala leo ameongoza Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala Afrika kwa njia ya mtandao.Mhe. Mchengerwa ameongoza Mkutano huo ili kupitia na kuidhinisha ajenda mbalimbali zilizowasilishwa na Mkutano wa Wataalamu uliofanyika tarehe 27 na 28 Aprili, 2021.
Miongoni mwa ajenda zilizopitiwa na kuidhinishwa ni rasimu ya Nyenzo ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Miiko na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala Afrika; ambapo iliridhiwa kuwa Tanzania, Afrika ya Kusini, Namibia, Cameroon na Kenya zitahusika katika kufanya majaribio ya Utekelezaji wa Nyezo husika.
Ajenda nyingine ni kuchagua Wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba; ambapo walioidhinishwa ni Mwenyekiti kutoka Afrika Kusini, Makamu Mwenyekiti wa Kwanza kutoka Algeria, Makamu Mwenyekiti wa Pili kutoka Cameroon, Makamu Mwenyekiti wa Tatu kutoka Benin na Katibu kutoka Tanzania.
Pia mkutano ulitathmini hali ya utiaji saini na uridhiwaji wa Mkataba wa Umoja wa Afrika na kupendekeza mbinu za kukuza uridhiaji wa pamoja wa Mkataba huo kwa nchi wanachama ambapo ilibainishwa kuwa, mpaka sasa mwenendo wa utiaji saini na uridhiwaji wa Mkataba miongoni mwa nchi wanachama, nchi 38 zimeshasaini, wakati nchi 19 tu zimeridhia na 19 zimewasilisha Nyaraka za kuidhinisha.
Aidha, Mkutano uliridhia juu ya kuhimiza Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kusaini na kuridhia Mkataba wa Umoja wa Afrika na Kuziomba AAPAM na AMDIN na Taasisi zingine kuutangaza Mkataba huu kupitia mijadala na tovuti mbalimbali.
Sanjali na hilo, wajumbe walipitia na kuridhia Azimio la Mkutano wa Pili wa Nchi Wanachama kwa kuwasilisha taarifa ya kwanza ya utekelezaji wa Mkataba kwa Kamishna wa Umoja wa Afrika ifikapo mwezi Januari, 2022, na kuiomba Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuandaa taarifa ya jumla kuhusu Utendaji wa Utumishi wa Umma katika Afrika ikiwa ni pamoja na kudumisha ushirikiano na mshikamano baina ya Nchi Wanachama.
Mkutano kazi huo, ulihudhuriwa na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika walioridhia Mkataba huu ambao ni Algeria, Benin, Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Mali, Namibia, Rwanda, Afrika ya Kusini, Mali, Ivory Coast, na Tanzania. Mkutano wa Tatu wa Nchi Wanachama utafanyika mwezi Aprili, 2022.
No comments:
Post a Comment