Pages

Wednesday, March 31, 2021

TANZANIA IKO SALAMA NA TUTAVUKA SALAMA-DKT TULIA

 Hotuba fupi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson wakati akitoa mchango wake kwenye Azimio la Bunge la kutambua mchango na kuenzi maisha ya Rais wa tano wa Tanzania hayati, Dr. John Magufuli na utumishi wake uliotukuka pamoja na Azimio la Bunge kumpongeza Samia Suluhu kuwa Rais wa sita wa Tanzania lililofanyaka Bungeni Dodoma leo March 30, 2021.


Dr. Tulia amesema“Safari hii tutafika salama, Mama yetu Samia Suluhu uliandaliwa vizuri kuwa

Rais wa Tanzania, kwa utumishi ambao aliufanya kwa kushirikiana na mtangulizi wake hayati Magufuli na sasa Mama anaifanya safari kwa kushirikiana na Dr. Mpango watakwenda vizuri”- Dr. Tulia Ackson

“Tanzania iko salama, iko katika mikono salama na tutavuka salama huko tunakotaka kweda na hatuna haja ya kuwa na shaka. Katika mambo yote haya tujifunze mambo mawili ambapo kwanza, kama viongozi na kama wananchi ni vizuri sana kuheshimiana kwasababu hatuifahamu kesho yetu.”- Dr. Tulia Ackson

“Pengine wapo watu walikuwa wanamtazama Makamu wa Rais kama ataendelea kuwa Makamu hivi… na sasa ameshakuwa Rais na hili ni funzo kwetu sote kuheshimu kila mtu umuonaye kwasababu huifahamu kesho yako.”- Dr. Tulia Ackson

“Jambo la pili na la mwisho ni kwamba wanadamu hatutadumu milele, ni vizuri kujitahidi kuufanya utumishi wako wakati huu na usisubiri kesho maana kesho sio yako na sisi sote humu ndani ni watumishi wa wale waliotuchagua hivyo tujitahidi kuwapa utumishi uliotukuka ili na sisi yumkini tuwe tumejifunza kwa maisha haya mafupi ya Dr. John Magufuli na sasa tukiungana kwa pamoja kumuunga mkono Rais wetu mpya Mama Samia”-Dr. Tulia Ackson



 

 

No comments:

Post a Comment