Moja ya post za itel ukurasa wa instagram iliyokuwa ikiwataka wafuasi wake kutabiri ni msanii gani.
Simu hiyo itakayozinduliwa na msanii huyo ambaye jina lake bado halijatajwa, ni simu yenye fasheni ya waterdrop na plus na ni full screen. Simu hiyo itakayouzwa kwa bei nafuu inatarajiwa kusambazwa nchi nzima katika maduka ya simu.
Taarifa za chinichini kutoka Kampuni ya simu za mkononi ya itel zinaeleza kuwa mwezi Aprili kampuni hiyo itazindua rasmi simu mpya ambayo itakwenda sambamba na kumtangaza balozi wake wa itel kwa mwaka 2021.
Ingawa taarifa hizi hazijathibitishwa rasmi, kuna chanzo ndani ya kamunii hiyo ambacho
kimedokezea taarifa hizi.“Mwezi Aprili itel imejiandaa kuzindua rasmi simu yake mpya toleo la A’series lakini kikubwa ni kwamba tutamtangaza balozi wetu wa itel kwa mwaka 2021, balozi huyu ni msanii mkubwa sana Afrika” kimedokeza chanzo hicho.
Pamoja na kutotaja jina la msanii huyo,katika kurasa za itel za Instagram na Facebook imeelezwa kuwa balozi huuyo ni msanii wa muziki aina ya afro beat, afro pop na bongo flava pia.
Hii ni miongoni mwa post kutoka ukurasa wa itel Tanzania Instagram iliyoelezea kuwa msanii huyo anajihusisha na sanaa ya muziki aina ya afro beat, afro pop na bongo flava.
Ikumbukwe kuwa itel Tanzania imewahi kuwa na balozi ambaye ni mwigizaji wa bongo muvi Bi. Irene Uwoya na kushirikiana naye katika kunadi bidhaa zake mwaka 2017. Je, safari hii ni nani anayezungumziwa katika minong’ono inayoendelea?
Ili kujua nani ni nani, yupi atakuwa balozi wa itel na atatangazwa lini, fuatilia taarifa zetu hapa tutaendelea kukujuza na pia unaweza kufuatilia kurasa za itel Instagram, Facebook na twitter kwa jina la itel Tanzania au bofya hapa: https://www.instagram.com/iteltanzania/
No comments:
Post a Comment