Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akili akifungua Mkutano wa pili wa Jukwaa la Bajeti na Uchumi la mwaka 2021/22 uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Zanzibar liliopo Kinazini.
Baadhi ya Makatibu wakuu na manaibu wao waliohudhuria katika Jukwaa la Bajeti na Uchumi wakifuatilia hutuba ya Katibu Mkuu Afisi ya Rais Fedha Dkt. Juma Malik Akili.
Afisa Uchumi katika Idara Uchumi Saleh Daadi Muhammed akiwasilisha mada ya mapitio na mwelekeo wa hali ya uchumi na mpango wa maendeleo katika jukwaa la bajeti lililofanyika Benki Kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama cha Watembezaji Watalii ya (ZATO) Omar Makame Kali akichangia mada alishauri kuwepo mfuko maalum wa kutangaza utalii katika bajeti ijayo.
Picha na Makame Mshenga.
**************************************************
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akili amewataka Wadau wa Jukwaa la Bajeti na Uchumi kushirikiana na Serikali katika kuandaa
Bajeti itakaweza kuwasaidia Wananchi.
Akifunguwa Mkutano wa Jukwaa la Bajeti na Uchumi kwa Serikali kuu huko katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Ofisi ya Zanzibar Kinazini amesema Jukwaa hilo,limeundwa na Taasisi mbalimbali litaweza kutoa mchango mkubwa katika kuwezesha Serikali kuandaa Bajeti yake itakayokwenda sambamba na mahitaji ya wananchi.
Amesema Serikali itaendelea kuthamini michango inayotolewa na Wadau hao katika kuhakikisha Bajeti hiyo inagusa na kuimarisha maisha ya wananchi katika kufikia malengo ya Serikali ya Uchumi wa Buluu.
Dkt. Malik amelitaka Jukwaa hilo kushirikiana na Taasisi zote ili kuepuka matatizo kwa baadhi ya taasisi nyengine kutoshirikishwa katika uandaji wa Bajeti hiyo.
Akiwasilisha Mada ya Mpitio na Muelekeo wa hali ya Uchumi na Mpango wa Maendeleo Afisa Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Saleh Saad Muhammed amesema hali ya uchumi umekuwa ukilinganisha na miaka iliopita na kuwaomba wadau hao kuzidi kushirikiana ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya nane.
Nao washiriki wa Mkutano huo wameiomba Serikali kuyapa kipao mbele masuala ya Utalii kwa kuyatangaza ndani na nje ya nchi pamoja na kuweka Mfuko maalum wa kuitangaza biashara hiyo.
No comments:
Post a Comment