Pages

Tuesday, February 2, 2021

MAHAKAMA YAANZISHA MFUMO WA TEHAMA AMBAO UTASAIDIA KUENDESHA KESI KWA URAHISI MKOA NJOMBE By Emmanuel Mbatilo - February 2, 2021 0 ******************************************8 Na Damian Kunambi, Njombe. Katika kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa mahakama ya kwanza hapa nchi 1921 mahakama imeweza kupiga hatua katika kuendesha mashauli yake ambapo imeanzisha mfumo wa tehama ambao utasaidia kuendesha kesi hizo kwa urahisi zaidi. Hayo ameyasema hakimu mkazi mfawidhi wa mahaka ya wilaya Ludewa iliyopo mkoani njombe Amon Kahimba katika maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambayo kiwilaya imeadhimishwa katika ukumbi wa halmashauri hiyo huku kimkoa ikiadhimishwa mkoani Dodoma. Amesema mfumo huo tayari umekwishaanza kutumika ambapo mtu anayetaka kufungua kesi anaweza kufungua kesi yake akiwa mahali popote nchini kwa kutumia mtandao pamoja nakuwawezesha kujua tarehe ya kusomwa kwa kesi zao. Ameongeza kuwa huduma hiyo ya tehama kwa upande wao ni msaada mkubwa kwakuwa inawawezesha kumhoji mtuhumiwa aliyeko mahabusu kwa kupitia mtandao pasipo kufika mahakani. “mfumo huu wa tehama unatusaidia kutenda haki kwa wakati hivyo imeleta mapinduzi katika utoaji haki kutoka nadharia kwenda kwenye vitendo na kupelekea benki ya kuhifandi hukumu kufanya kazi kiufasaha”, Amesema Kahimba. Aidha kwa upande wa mkuu wa wilaya hiyo Andrea Tsere ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ameipongeza mahakama kwa uendeshaji wa mashauri kwa kutumia tehama na kuongeza kuwa anatamani mfumo huo ungetumika hata kwa idara nyingine pia kama jeshi la polisi. Amesema jeshi la polisi linapaswa kujifunza mfumo wa namana hiyo ili kuweza kufanya upelezi kwa wakati kwani kumekuwa na ucheleweshaji wa kutoa hukumu katika kesi mbalimbali kutokana na upelelezi kutokamilika kwa wakati. “OCD nafikiri umesikia kwa jinsi gani mahaka imeweza kutumia mfumo wa tehama kama njia ya kurahisisha kazi zao na kuwapa wananchi huduma kwa urahisi zaidi, nanyi pia mnapaswa kuiga mfumo huu ili muweze kufanya upelelezi kwa urahisi maana kesi nyingi upelelezi wake unachelewa kukakamilika hasa kwa kesi za mauaji.

MAHAKAMA YAANZISHA MFUMO WA TEHAMA AMBAO UTASAIDIA KUENDESHA KESI KWA URAHISI MKOA NJOMBE


******************************************8

Na Damian Kunambi, Njombe.

Katika kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa mahakama ya kwanza hapa nchi 1921 mahakama imeweza kupiga hatua katika kuendesha mashauli yake ambapo imeanzisha mfumo wa tehama ambao utasaidia kuendesha kesi hizo kwa urahisi zaidi.

Hayo ameyasema hakimu mkazi mfawidhi wa mahaka ya wilaya Ludewa iliyopo mkoani njombe Amon Kahimba katika maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambayo kiwilaya imeadhimishwa katika ukumbi wa halmashauri hiyo huku kimkoa ikiadhimishwa mkoani Dodoma.

Amesema mfumo huo tayari umekwishaanza kutumika ambapo mtu anayetaka kufungua kesi anaweza kufungua kesi yake akiwa mahali popote nchini kwa kutumia mtandao pamoja nakuwawezesha kujua tarehe ya kusomwa kwa kesi zao.

Ameongeza kuwa huduma hiyo ya tehama kwa upande wao ni msaada mkubwa kwakuwa inawawezesha kumhoji mtuhumiwa aliyeko mahabusu kwa kupitia mtandao pasipo kufika mahakani.

“mfumo huu wa tehama unatusaidia kutenda haki kwa wakati hivyo imeleta mapinduzi katika utoaji haki kutoka nadharia kwenda kwenye vitendo na kupelekea benki ya kuhifandi hukumu kufanya kazi kiufasaha”, Amesema  Kahimba.

Aidha kwa upande wa mkuu wa wilaya hiyo Andrea Tsere ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ameipongeza mahakama kwa uendeshaji wa mashauri kwa kutumia tehama na kuongeza kuwa anatamani mfumo huo ungetumika hata kwa idara nyingine pia kama jeshi la polisi.

Amesema jeshi la polisi linapaswa kujifunza mfumo wa namana hiyo ili kuweza kufanya upelezi kwa wakati kwani kumekuwa na ucheleweshaji wa kutoa hukumu katika kesi mbalimbali kutokana na upelelezi kutokamilika kwa wakati.

“OCD nafikiri umesikia kwa jinsi gani mahaka imeweza kutumia mfumo wa tehama kama njia ya kurahisisha kazi zao na kuwapa wananchi huduma kwa urahisi zaidi, nanyi pia mnapaswa kuiga mfumo huu ili muweze kufanya upelelezi kwa urahisi maana kesi nyingi upelelezi wake unachelewa kukakamilika hasa kwa kesi za mauaji.

 

No comments:

Post a Comment